[wanabidii] MDAHALO KUJADILI UMUHIMU WA KUZINGATIA MAMBO YA MSINGI KATIKA MCHAKATO WA KUPATA KATIBA MPYA, JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014

Sunday, August 03, 2014
MDAHALO    MDAHALO   MDAHALO   MDAHALO
JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014, Blue Peal Hotel, Ubungo Plaza
kuanzia saa 9.00 mchana hadi 12.00 jioni


 
Taasisi ya Mwalimu Nyerere imeandaa mdahalo kujadili umuhimu  wa kuzingatia mambo ya msingi katika mchakato wa kupata Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 
Wazungumzaji katika mdahalo huu ni pamoja na waliokuwa Makamishna wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba: Jaji Joseph S. Warioba, Mwenyekiti wa Tume, Dr. Salim Ahmed Salim, Mzee Joseph W. Butiku, Bi Mwantumu Malale, Prof. Palamagamba Kabudi, Ndugu Awadh Ali  Saidi, na Ndugu Humphrey Polepole. 


Wananchi wa kawaida na viongozi kutoka taasisi na asasi mbalimbali. zinazowakilisha jamii ya Watanzania ambazo ni pamoja na asasi za kiraia (NGOs), vyama vya siasa, madhehebu ya dini, wasomi, vyombo vya habari, taasisi za kitaaluma, vyama vya ushirika vya wakulima na wafugaji, vyama vya wafanyakazi,  n.k nyote mnakaribishwa.


                                 Muda na Mahali: JUMATATU TAREHE 4 AGOSTI 2014, kuanzia saa 8.30 mchana hadi 12.00 jioni,                         
                                              Blue Peal Hotel, Ubungo Plaza.    
                                            
Mdahalo utarushwa moja kwa moja na television ya ITV.

NYOTE MNAKARIBISHWA.

Edgar Atubonekisye
Assistant Programmes Officer, The Mwalimu Nyerere Foundation
+255 754 988 946

 

Share this :

Related Posts

0 Comments