[wanabidii] ITV KUCHUKULIWA HATUA ETI KWA KURUSHA MIDAHALO YA KATIBA

Tuesday, August 05, 2014
ITV KUCHUKULIWA HATUA ETI KWA KURUSHA MIDAHALO YA KATIBA.

Bunge la Katiba limeanza kazi Dodoma, jambo la kusikitisha ni kuwa wameacha kazi ya msingi ya kujadili matakwa ya CCM kikatiba na wanajadili UKAWA.

Mwanahabari rafiki yangu na ninayemheshimu sana #Hamis#Dambaya# mwakilishi wa Wakulima anasema kuwa Samwel Sitta atafute namna ya kuzuia kina Jaji Warioba wasiongelee masuala ya katiba nje ya bunge Maalum. Leo mwandishi nguli anatumika kuhujumu haki na uhuru wa wananchi kupashana habari kwa njia za amani.

Samweli Sitta anakoleza moto na kumjibu Dambaya kuwa tatizo kubwa ni ITV, kwamba imeacha kabisa kazi ya kutangaza habari na sasa inajishughulisha na midahalo maalum tu. Mhe. Samwel Sitta anaishangaa serikali kwa nini hadi sasa haiichukulii hatua ITV. Huyu mzee naye anapambana kutafuta urais wa nchi huku hana hata chembe ya uvumilivu wa kusikia mawazo mbadala yanayorushwa na vyombo vya habari.

Sasa Bunge la Katiba linaanza ku-HUNT(KUWINDA) chombo kipi cha habari kinarusha mawazo dhidi ya Bunge la Katiba. Mzee Samwel Sitta atambue kuwa ana wajibu mkubwa sana, kama ana watu wanamshauri wakamshauri vema. Karne hii dhamira yake mbaya itashindwa.



Julius Mtatiro,
Dar Es Salaam.

Share this :

Related Posts

0 Comments