[wanabidii] Wajumbe Bunge Maalum kupigania usawa na mgawanyo wa rasilimali

Friday, July 25, 2014
[caption id="attachment_48981" align="aligncenter" width="480"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0835.jpg" alt="Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Fedrick Msigala akizungumza na wanahabari mara baada ya Mkutano wao na Mtandao wa Wanawake na Katiba uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam." width="480" height="599" class="size-full wp-image-48981" /> Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Fedrick Msigala akizungumza na wanahabari mara baada ya Mkutano wao na Mtandao wa Wanawake na Katiba uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_48983" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0814.jpg" alt="Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam." width="640" height="430" class="size-full wp-image-48983" /> Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_48985" align="aligncenter" width="480"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0792.jpg" alt="Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akiongoza majadiliano katika Mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mtandao wa Wanawake na Katiba." width="480" height="588" class="size-full wp-image-48985" /> Mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya akiongoza majadiliano katika Mkutano wa Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mtandao wa Wanawake na Katiba.[/caption][caption id="attachment_48984" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0799.jpg" alt="Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam." width="640" height="373" class="size-full wp-image-48984" /> Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_48986" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0786.jpg" alt="Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam." width="640" height="404" class="size-full wp-image-48986" /> Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam.[/caption][caption id="attachment_48982" align="aligncenter" width="640"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/07/IMG_0816.jpg" alt="Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam." width="640" height="427" class="size-full wp-image-48982" /> Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wakiwa katika majadiliano katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam.[/caption]

<strong>WAJUMBE</strong> wa Bunge Maalumu la Katiba walioshiriki katika mkutano wa majadiliano uliondaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba wameahidi kupaza sauti kupigania masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia pamoja na kusimamia usawa kwa jamii yote juu ya mgawanyo wa rasilimali ardhi, elimu, uongozi na huduma za kijamii.

Kauli hiyo imetolewa leo na baadhi ya wajumbe hao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari, katika Hoteli ya Golden Tulip ya jijini Dar es Salaam eneo unapofanyika mkutano huo uliomalizika leo jioni. Mjumbe wa Bunge Maalum, Valerie Msoka alisema majadiliano walioshiriki yamewawezesha wajumbe kurudi katika majadiliano ya awamu ya pili wakiwa na nguvu mpya huku wakiyapa kipaumbele na kuhakikisha kuna usawa katika masuala ya ardhi, elimu, rasilimali, uongozi na huduma za kijamii.

Alisema kwa muda wa mwanzo ambao wajumbe walipata kuhudhuria na kujadili baadhi ya ibara wamepata uzoefu kidogo jambo ambalo kwa kipindi cha pili litawasaidia kuongeza ujasiri wa kuendeleza hoja zao za msingi zikiwemo walizoshiriki kuzijadili katika mkutano huo. Kwa upande wake Mjumbe wa Bunge Maalum, Fedrick Msigala alisema mkutano huo umewawezesha wajumbe kujenga zaidi uelewa juu ya masuala ya usawa wa jinsia na kuangalia namna wajumbe wanaweza kuyatetea kuingizwa kwenye mchakato wa uundaji katiba mpya unaoendelea.

"…Mimi kama mwakilishi wa walemavu natambua namna ambayo wanawake walemavu wanavyo athirika na vitendo vya ukatili na manyanyaso yote ambayo wanakumbana nayo…sasa semina kama hii inatupa taarifa na uwezo pia wa kujenga hoja katika kutetea usawa wa kijinsia kuingizwa vizuri kwenye ibara mbalimbali husika kwenye Katiba Mpya," alisema Msigala.

Naye mjumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba, Usu Mallya alisema majadiliano hayo kati ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba na Wajumbe wa Mtandao wa Wanawake na Katiba ni nafasi muhimu kwani inawakumbusha wajumbe kupaza sauti juu ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia kuingizwa kwenye sheria mama ya nchi ambayo ni katiba.

Alisema masuala ya haki za wanawake na usawa wa kijinsia yakiingizwa katika jamii yataziwezesha mamlaka husika kuwajibika na taasisi husika kusimamia kwa uhakika na kuziwajibisha pale masuala hayo yanaposhindwa kutekelezwa kwa mujibu wa maelekezo.
"…Muhimu pia ni kutambua umuhimu wa kusimika suala la usawa wa kijinsia kwenye katiba ni kutokana na ukweli kwamba wanawake wanahusika katika kulikamilisha taifa la Tanzania na wanamchango mkubwa licha ya mfumo kuendelea kuwabana katika fursa mbalimbali," alisema Bi. Mallya.

Alisema sasa umefika wakati fikra potofu zitokomezwe ambazo zimekuwa zikiendelea kuwabana wanawake kwamba hawawezi na kuambulia nafasi ndogondogo maeneo anuai ya vyombo vya maamuzi ngazi zote.

"Nafasi kama hii ya kuwezesha Wajumbe wa Bunge la Katiba waweze kuendelea kuyabeba haya masuala katika mjadala utakaoendelea ni muhimu…na kwetu sisi tunachotegemea ni kwamba haya masuala yataendelea kuwa ni sehemu ya msingi katika majadiliano yanayoendelea kule bungeni, tunawaomba waandishi wa habari waendelee kuzipa nafasi hizi hoja na tunawapongeza pia kwa kutuunga mkono," alisema Bi. Mallya.

Mkutano huo umetoka na maadhimio ambayo wajumbe wataendelea kuyafanyia kazi, ikiwemo washiriki kuendelea kuwasiliana na kupanua wingo wa kupaza sauti juu ya hoja walizozijadili na kuyashirikisha makundi mengine katika kupaza sauti ili hoja zilizojadiliwa zipate nafasi ya kuingizwa kwenye mchakato.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com

--
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments