[wanabidii] VIGOGO WA CHADEMA MKOA WA TABORA WAHAMIA ACT TANZANIA

Tuesday, July 22, 2014
WIMBI la viongozi wa Chama kinachojiita cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kukikimbia chama hicho ziliendela leo mkoani Tabora, kufuatia Katibu wa Chama hicho  mkoani humo Othman Balozi naye kutangaza kubwaga Manyanga na kujiunga na chama kipya cha  ACT Tanzania.
 
Habari tulizopata kwa simu kutoka kwa wadau mkoani Tabora, zimesema kwamba, mbali na Balozi aliyewaongoza wajumbe 78 wa baraza kuu la Chadema hivi karibuni kwenda kwa msajili wa vyama kulalamikia katiba ya Chadema kukiukwa, pia wamo viongozi mbali mbali wa mabaraza ya kimkoa kiwilaya na majimbo walioamua kujitoa na kujiunga na Chama kipya cha ACT-Tanzania ambacho kinaaminika kuanzishwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe (Mbunge-Chadema).
 
Viongozi hao ni mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa  Tabora Hussein Kundecha,mratibu wa uhamasishaji Bavicha  wilaya ya Tabora mjini Nzuki Machibya na Ramadhan Simba Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Bukene.
 
Wengine ni Suni Yohane aliyewahi kuwa katibu wa Chadema wilaya ya Nzega pamoja na mwenyekiti wa baraza la wanawake katika wilaya hiyo.
 
Wimbi hilo pia limewazoa wanachama wa kawaida kutoka Chadema na CUF pamoja na watu 200 ambao  hawakuwahi kuwa wanachama wa chama chochote hapo awali.
 
Kuhama kwa viongozi hao kumekuja ikiwa ni siku moja baada ya waliokuwa viongozi wa Chama hicho mkoa wa Kigoma kubwaga Manyanga
 
Waliobwaga Manyanga kwa Mkoa wa Kigoma hiyo juzi ni Jafari Kasisiko Mwenyekiti, katibu Msafiri Wamalwa na iti wa Baraza la wanawake wa  mkoa wa Kigoma kubwaga Manyanga
 
Akizungumzia sababu ya kujiondoa Chadema Balozi alisema kabla ya kufikia uamuzi huo alimpa taarifa mwenyekiti wake wa mkoa Kansa Mbaruku juu ya uamuzi huo
 
Alisema akiwa miongoni mwa viongozi wa awali kukipokea Chadema katika mkoa wa Tabora,amechoshwa na chama hicho kuacha misingi yake ya  kidemokrasia na kukumbatia Ubabe na dharau huku wakiwanyooshea vidole  vya usaliti wale wanaohoji baadhi ya mambo wasiyoridhika nayo ndani ya Chama hicho.
 
"Leo mimi ni mtu huru na nimewasikiliza ACT na falsafa yao ya uwazi na kuamua kujinga kwa hiari yangu sasa huu uwazi waudhihirishe na sitasita kuhoji pale penye matatizo nawasihi katika hali hiyo wawe wavumilivu kwa tutakayohoji"alisema Balozi.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments