UJUMBE MFUPI WA MANENO NA HAKI ZA MTEJA
Wengi wetu tumewahi kupokea ujumbe mfupi wa maneno yaani SMS bila wenyewe kutaka halafu hapo hapo utaona kiasi Fulani cha hela kimeondoka kutokana na ujumbe huu , wakati mwingine simu haina hela lakini unapoingiza hela tu ujumbe utaingia na hela utakatwa .
Baadhi ya nchi wameanza kufikishana mahakamani kutokana na aina hizi za SMS za Promosheni , watu wanataka haki zao za mawasiliano zimeshimiwe na waamue wenyewe kama wanataka kujiunga kwenye huduma au la .
Mwanasheria mmoja nchini Uganda ameifikisha mahakamani kampuni ya MTN Uganda kwa tuhuma za kumtumia ujumbe mfupi yaani SMS wa matangazo , Mwanasheria huyu anataka kampuni ya MTN Uganda kuacha mara moja kumtumia ujumbe mfupi wa matangazo mara moja .
Amesema yeye ni mtumiaji na amesajiliwa kutumia simcard ya mtandao wa MTN Uganda anataka mahakama itamke kwamba Utumaji huo wa MTN Uganda ni uvunjaji wa haki zake .
Mahakama imeitaka kampuni ya MTN Uganda kuwasilisha utetezi wake ndani ya Siku 15 toka shauri hilo kupelekwa mahakamani .
Kabla ya suala hili la mahakamani , taasisi inayohusika na usimamizi wa mawasiliano nchini Uganda , UCC , Uganda Communications Commision , ilipiga marufuku utumaji wa ujumbe mfupi wa matangazo kwa watumiaji wa huduma za simu nchini humo , marufuku hii ilianza kutumika toka tarehe 8 juni mwaka 2014 .
UCC imetaka kampuni zote za mawasiliano nchini Uganda kuandaa utaratibu wa jinsi watakavyoendesha huduma kama hizo bila kusumbua watumiaji wa huduma za mawasiliano haswa kwenye suala la Ujumbe mfupi .
Pamoja na yote hayo kuna masuala kama 3 ambayo wateja wengi wamekuwa wanalalamika ambayo yanafanana katika sehemu nyingi haswa hapa nchini .
Moja ni mkataba au makubaliano kati ya mtumiaji wa namba husika na mtoa huduma wake , kwamba hakuna mkataba rasmi ambao unatamka rasmi kwamba mteja amekubali mwenyewe kutumia SMS za matangazo au zozote toka kwa mtoa huduma ,kuna takiwa mkataba kama huu ili mteja aamue mwenyewe kama anataka kujiunga au la .
Pili ni suala la kampuni za simu kutumia mwanya huo wa kutokuwa na mkataba kuanzisha promosheni na kuzituma kwa wateja wake kwa sababu ya sheria mbovu za mawasiliano au kutokuwa na kipengele hicho kabisa kwenye sheria ya usimamizi wa mawasiliano .
Kutokana na suala hili la Nchi jirani ya Uganda ni vizuri hapa kwetu tujiandae kujadili suala hili kama sheria ya mawasiliano haijapelekwa bungeni kwa ajili ya mjadala na kitu hiki kiangaliwe ili kuweza kulinda maslahi ya mteja .
Inajulikana wazi jinsi kampuni za mawasiliano zinavyopata faida kubwa kutokana na ujumbe mfupi wa maneno na suala hili linaweza kuharibu faida zao , lakini ni vizuri mteja apewe haki yake ya kuamua kama anataka kupokea ujumbe kama hiyo au la au kuwe na utaratibu wa kuchagua aina ya ujumbe mfupi anaopenda kujiunga pindi anaponunua laini ya simu .
Hili suala hata hapa nchini limekuwa linapigiwa sana kelele na watumiaji kadhaa wa mitandao ya simu lakini baadhi ya watendaji wa kampuni hizo husema wanaotuma matangazo hayo sio wao bali ni wateja wao , wao kama kampuni wanawezesha matangazo kutumwa tu na kulipwa ujira wao .
Kwenye sheria ya Mawasiliano kuna kipengele cha Privacy Act , hiki ndio kinahusika na masuala binafsi ya kila mtumiaji wa huduma za mawasiliano na hapo ndio tutaweza kuongezea kipengele hiki cha Matangazo au promosheni .
YONA FARES MARO
0786 806028
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments