[wanabidii] TANZANIA HATUHITAJI KIJANA...TUNAHITAJI RAISI

Sunday, July 06, 2014

kumeibuka baadhi ya wanasiasa na makundi yao ya kuwaunga mkono katika harakati zao za kuusaka uraisi wa jamuhuri yetu, WANAFANYA VEMA SANA. Lakini chakushangaza na kusikitisha ni kuwa wanatumia HOJA DHAIFU YA UJANA vs UZEE KUHALALISHA UCHU WAO badala ya HOJA ZENYE MASHIKO. Wanadai eti Tanzania ya sasa inahitaji kijana mwenye mawazo mapya..sijui na madudu gani mengine wanayoyajua wao.

NANI AMEWAAMBIA kuwa kijana ndio sifa ya kuukwaa uraisi? Vijana wote wana mitizamo mipya?
NANI AMEWAAMBIA kuwa mzee na akili pia zimezeeka? Hakuna wazee wenye busara, hekima, ujuzi wa kutosha na maarifa kuongoza?

ANGALIZO:
1. Hizi ni hoja za kibaguzi ambazo hazitusaidii. Zipo nchi nyingi ambazo zinaongozwa na wazee na mambo yanaenda. Tanzania hatuhitaji kijana ili mambo yaende au mzee.

TUNAHITAJI RAISI AMBAYE, anabeba ajenda za wananchi, mtizamo sahihi kuhusu maendeleo ya taifa, mwenye kupunguza ombwe la walionacho na wasionacho kwa kuja na njia mbadala, mwenye kuweka maslahi ya taifa mbele na sio chama chake au umaarufu wake. Hivyo hoja ya ujana au uzee sio hoja muafaka kwa Tanzania yetu

MUNGU IBARIKI TANZANIA

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments