TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa leo imepokea taarifa kutoka Ubalozi wa Libya hapa nchini kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya, Bwana Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa Saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Lbya.
Inataarifiwa kuwa Bwana Nwairat alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto. Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlipuko wa
bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini. Walimkimbiza hospitali ya AMI Oysterbay ambako alitangazwa kuwa alikwisha kufariki na Polisi walithibitisha kifo hicho.
Maiti imehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu Nwairat kwenda Nyumbani kwa mazishi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeuhakikishia Ubalozi wa Libya Ushirikiano wake katika kipindi hiki kigumu.
IMETOLEWA NA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Dar es Salaam
Julai 2,2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments