July 30 imesambaa Taarifa ya ajali ambayo imetokea mapema leo na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma ajali iliyosababisha vifo vya watu 17 kati yao wanaume 12, wanawake 5 na majeruhi kwa mujibu wa jeshi la Polisi Dodoma.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 08:00 asubuhi eneo la Pandambili barabara ya Dodoma –Morogoro ambayo imehusisha basi la kampuni ya Moro Best yenye namba T258 AHV ambalo lilikuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam.
Basi hilo lilikuwa likiendeshwa na SAID S/O LUSOGO liligongana na Lori namba T820CKU / T390CKT lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma likiendeshwa na GILBERT S/O ISAYA NEMANYA.Taarifa ya kamanda wa Polisi inseam katika ajali hiyo watu 17 wamepoteza maisha kati yao wanaume ni 12 na wanawake ni 5. Pia watu 56 wamepata majeraha mbalimbali na wamelazwa katika Hospitali za wilaya ya Kongwa na Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma. Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na dereva wa lori hilo pamoja na utingo wake.
Chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kutokuwa na tahadhari kwa magari yaliyokuwa yanakuja mbele yake wakati anapita (overtake) gari lingine na kwenda kuligonga busi hilo
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments