[wanabidii] Taarifa kuhusu Kamati Maalum ya Kamati ya Mashauriano ya Bunge Maalum

Tuesday, July 15, 2014
Monday, July 14, 2014
Kamati maalum ya kamati ya mashauriano ya Bunge la Katiba Tanzania liatarajia kukutana kutathmini kazi zilizofikiwa za utungaji wa Katiba Mpya ya Tanzania.

Kamati hiyo inatarajiwa kukutana kwa siku mbili kuanzia tarehe 24 mwezi huu katika Ofisi ndogo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Bunge hilo Maalum la Katiba Mhe. Yahya Khamis Hamad 
imeeleza kuwa kamati hiyo inawajumuisha wajumbe thelathini walioteuliwa na Mwenyekti wa Bunge hilo Mhe Samwel Sita na Makamu wake Mhe Samia Suluhu Hassan.

Uteuzi wa wajumbe wa Kamati hiyo ya mashauriano ya Bunge imeteuliwa chini ya masharti ya kanuni ya 54(4) na (5) ya kanuni za Bunge Maalum za mwaka 2014.

Taarifa hiyo imewaomba wajumbe walioteuliwa kuhuduhria kikao hicho kwa lengo la kufanikisha kazi waliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa niaba ya Watanzania.

Himid Choko, BLW

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments