[wanabidii] SHAIRI: NI UGONJWA AU SHIDA, UPUNGUFU WA FIKRA?

Wednesday, July 23, 2014

Ni ugonjwa au shida , upungufu wa fikra?

Kahabi G Isangula, Dar, Tanzania, kaisa079@gmail.com

Kisima Cha Mashairi

Lanikwaza jambo hili, moyowane waumia
Sidhani wastahili, kuchuuza ka bamia
Kujivika mibangili, midume kuhudumia
Ni ugonjwa au shida, upungufu wa fikra?

Huwekeza kwa urembo, kucha na Rangi za Nywele
Hujivika umgambo, kuranda huku na kule
Hubadili mitalimbo, paso ogopa upele
Ni ugonjwa au shida, upungufu wa fikra?

Huzuzuka kwa magari, hasa yenye viyoyozi
Huzoa wanyamapori, uroda kwao ni 'kazi'
Heshima siyo habari,mambo ya utandawazi
Ni ugonjwa au shida, upungufu wa fikra?

Moyowane waniuma, madada wapenda poa
Hapa mtaa wa nyuma, manguli kujipodoa
Jioni wanatupima, kama tutawaopoa
Ni ugonjwa au shida,upungufu wa fikra?

Kwani lazima kuuza, ya mwiliwe starehe?
Mahubiri kuyabeza, na mafunzo ya Mashehe
Visingizi kuteleza, 'kuchuna' kwenu sherehe
Ni ugonjwa au shida, upungufu wa fikra?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments