[wanabidii] SERIKALI 'KUYAPIGA KUFULI' MAKANISA YENYE MIGOGORO KUNUSURU AMANI

Monday, July 28, 2014
Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani. 

Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. 

Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema "Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari". 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto) akiungana na maelfu ya Waumini wa Karismatiki Katoliki, Jimbo la Dar es Salaam katika maombi maalumu kwa ajili ya kuliombea Taifa. 

Maombi hayo yalifanyika katika Kituo cha Karismatiki, Ubungo jijini Dar es Salaam jana. 

Waziri Chikawe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maombi hayo aliyataka Makanisa nchini kudumisha amani na utulivu na kuendelea kuliombea Taifa na kuepuka kuingia katika migogoro mbalimbali ambayo itasababisha taifa kuingia katika uvunjifu amani makanisani.

Aidha, Chikawe aliongeza kuwa migogoro katika Makanisa na Madhehebu mbalimbali nchini imekuwa mingi katika kipindi hiki ambapo migogoro hiyo inasababishwa na ubinafsi wa viongozi, kutofuata Katiba na Ubadhirifu wa mali za Kanisa. 

Kutokana na migogoro hiyo Chikawe alisema; "Serikali haitavumilia vitendo vya uvunjifu wa amani makanisani na ikibidi itafuta usajili wa madhehebu na makanisa yenye migogoro ili kuepusha shari". 

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI 

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments