[wanabidii] Mwanamuziki Jhikoman ameshatua Tubingen,Ujerumani kwa ajili ya Kutumbuiza

Wednesday, July 09, 2014







MWANAMUZIKI JHIKOMAN AMESHATUA TUBINGEN, UJERUMANI

ATATUMBUIZA NDANI YA 5th International African festival Tubingen 2014

Kutoka Bagamoyo ,Tanzania hadi Kimataifa ! Ujerumani Kutingishwa na Muziki!


Tübingen,Ujerumani

Mwanamuziki nyota wa reggae barani Afrika Jhiko Manyika aka Jhikoman kutoka Bagamoyo,Tanzania amewasili mjini Tubingen,Ujerumani kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho makubwa ya 5th International African Festival Tübingen 2014,yatakayoanza 17 julai 2014 mpaka 20 Julai 2014 katika viwanja ya Festplatz,mjini Tübingen. watayarishaji wa maonyesho hayo
Afrikaktiv.org wamemtaja mwanamuziki Jhikoman kuwa ni nyota inayong'aa kutoka Afrika na wamemwalika kwa ajii ya kuja kuzidisha mwangaza katika soko la ulaya. Mkurugenzi wa maonyesho hayo Madam Susan Tatah alisema kuwa ujio wa mwanamuziki Jhikoman nchini Ujerumani unazidisha uhusiano mzuri katika sekta ya sanaa na utamaduni kati ya Ujerumani na Tanzania pia Afrika kwa ujumla,Madam Susan Tatah alisema ujio wa Jhikoman una maana kubwa kwa wajerumani kwa mwanamuziki huyo anatoka katika mji wa Bagamoyo ambako ndipo palikuwa makao makuu ya serekali ya ukoloni ya kijerumani na ndipo wajerumani walipojenga shule ya mwanzo Afrika Mashariki, Madam Susan Tatah alisema Jhikoman pia atatia sahini
mkataba wa ushirikiano wa kudumu wa "Cultural Exchange program" pamoja Afrikaktive pia na mji wa Tübingen.





--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments