[wanabidii] Maamuzi Gani Nichukue Dhidi ya Ndoa Yangu?

Thursday, July 10, 2014

Mimi ni mama wa watoto wawili, nimefunga ndoa miaka saba iliyopita, mwanzo kabisa maisha yangu ya mahusiano hayakuwa mazuri hata kidogo, first of all niliwahi kubakwa nikiwa na umri wa miaka 15, baada ya hapo niliishi maisha ya tabu sana mpaka nilipokuwa mkubwa na kuweza kujitambua.

Nillianza maisha ya mahusiano nikiwa na miaka 21 na mwanaume niliyetokea kumpenda na kuamini yeye ndio atakayenifuta machozi na huzuni zangu.

Mambo hayakuwa hivyo kwani miaka miatatu ya mahusiano yetu alienda oversizi na kuniacha na pia kuamua kukata mawasiliano kabisa. Nilibaki na kovu na maumivu niliyokosa tiba. Nilimtafuta bila mafanikio na kuamua kumove on na maisha yangu,ingawa ilikuwa ni ngumu sana.

Baada ya hapo nilikutana na mwamaume ambaye sikujua kama ni kweli nampenda kwani siku zote nilipokuwa nae nilikuwa namuwaza X wangu aliyeniacha bila kusema neno lolote.
Mwanaume huyu mwanzo sikumuelewa kabisa kwanza alikuwa mgomvi na mkorofi kwa watu dakika mbili alishabadirika haeleweki kama kinyonga ,police kwake ilikuwa ni kama nyumbani.
Nyimbo zake mara nyingi zilikuwa ni za kina Tupac ,Snopy D na wale aina ya magang star Ingawa alikuwa msomi na kazi nzuri,na maisha yake mpaka sasa bado miziki yake ndio hiyo ,starehe kwake hataki kuacha wala kupunguza.
Niliamini atabadilika ingawa nilikuwa nakwazika sana kuwa nae alinifundisha kunywa Pombe ,Ok nikawa mnywaji mzuri na ili niwe nae Kimapenzi niliona ninywe kwanza ndio nakuwa huru na hayo ndio yakawa maisha yangu..Tuliendelea na mahusiano ya muda mrefu hatimaye nilianza kumzoealakini si kumpenda ,
Tukiwa tayari ndani ya mahusiano nilishika mimba na tukakubaliana kuanza kukaa pamoja ,taratibu za mahali zilifanyika na nikahama rasmi lakini kwa sababu jamaa alikuwa mtu wa starehe alikuwa akiniacha na kurudi usiku wa manane amelewa mara anitukane na sikuona kama alikuwa ananithamini na hali yangu ya ujauzito chuki moyoni ikawa inazidi siku hadi siku.
Ingawa kuna wakati nilikuwa naona kama ananipenda .Baada ya kujifungua tulianza taratibu za ndoa lakini moyoni mwangu nikijua kabisa mwanaume huyu sina mapenzi nae hata kidogo.Na nilikuwa najiuliza kwanini nafunga ndoa?
Ingawa kuna vitu vingine vilikuwa kama najifosi kufanya. Tulifunga ndoa takatifu nakuanza kuishi kama mke na mme ,na mungu akatujaalia kuongeza mtoto mwingine wa kiume lakini system yangu ni mpaka ninywe ndio nakuwa na hisia za kuwa na mme wangu.
Ndani ya ndoa yangu nimekuwa nikiishi kwa kujifanya nampenda mme wangu ingawa hizo hisia sijawahi kuzipata hata kidogo ,nimekuwa nikilia na kujutia maamuzi yangu sina furaha ,ni mnyonge ,for the sake of my kids ndio napata faraja kidogo.
Kila siku zinavyoenda nazidi kuchanganyikiwa mwenzenu nitaishi hivi mpaka lini nifanye nini ili nipate amani ya roho,? maana hii pretend sasa imenichosha. Nakosa usingizi usiku kucha.
Ni mengi ya kuelezea lakini kwa hapa moyo wangu unazidi kuwa mnyonge
Nisaidieni juu ya hili
By Ndoa Yangu

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments