[wanabidii] Democracy or Mockracy in Africa ?

Wednesday, July 09, 2014
Demokrasia  au Usimango Na Dhihaka Barani Afrika ? 
(Democracy or Mockracy in Africa ?)

Na Benn Haidari

Katika kipindi cha miaka zaidi ya 60 iliyopita wananchi wa nchi na mataifa mbali-mbali 
ya afrika,Asia na Latin Amerika  walipambana kwa njia kujitowa kwenye utawala wa Ki-imla
na ukoloni wakiwa na madai na tamaa ya kuwa huru na demokrasia.

Si katika wananchi wote katika nchi zilizopata uhuru walibahatika kuwa na utawala wa demokrasia .
Kiwango cha demokrasia au ukosefu wa hilo ulikuwa unatofautiana kutoka nchi na nchi;kwengine
ilikuwa ni bora wakati wa utawala wa Ki-imla na ukoloni kuliko wakati wa huo "uhuru wa nchi yao ".
Mifano ya ukosefu wa "Uhuru wa kweli na Deokrasia " ni mingi sana kote duniani si kitu kilichopo
katika nchi zetu tu barani afrika pekee .Ingawje huo ndio ukweli wa mambo,lakini hata hivyo wingi 
huo wa U-Imla hauhalalishi uovu na ukatili huo popote uliopo.

Demokrasia-Ufalme na U-Imla.

Inatambulika kwamba ,fasiri halisi ya mfumo wa demokrasi kuwa ni aina ya utawalaji/utaratibu wa
nchi ambao unapatikana kutokana na maazumi ya wengi wa wananchi kwa njia khasa za upigaji kura.
Kwa kifupi ni utawala ni utawala uliochaguliwa na wengi miongoni mwa wananchi wenye haki ya 
kupiga kura . Utawala wa Ki-falme na U-imla taratibu za haki kama hizo kwa wananchi hazipatikani.

Ufalme-U-imla na Mapinduzi.Vitu hivi vitatu navyo vinatafautiana.Ufalme ni utawala wa Kurithi.
U-Imla unafanana na Ufalme na mara nyingi unakuwa ni utawala wa mabavu wa wachache na kwa 
manufaa ya wachache hao. Mapinduzi ni mabadiliko ya ghafla ya ama kuubwaga Ufalme au U-Imla
wa aina tofauti kwa njia za umwagaji wa damu dhidi ya dhulma ,unyonyaji na unyanywasaji .
Mara nyingi Mapinduzi huwa yanafanywa na walalahoi waliochoshwa au hata kundi la tabaka fulani
ambalo halikubaliani na mfumo dhulma nchini.Tukichanganua Mapinduzi ya France,Marekani,Urussi 
na Industrial Revolution ya Uingereza - tunaweza kuona tofauti mbali-mbali na kundi gani la watu 
lillilo faida baada ya Mapinduzi .Kila Mapinduzi huleta dhiki na faraja zake .Mfano wa Mapinduzi ya
watu wa Iran,Egypt na ya Zanzibar nayo yana mengi ya kuchanganuliwa kwa kila namna na tofauti
zake - khasa kwenye suala la " Mapinduzi yaliwanufaisha na nani n verejee ?". Tathmini za yaliyo
fanyika baada ya Mapinduzi katika nchi hizo zina sura mbali-mbali,yote ikitegemea nani na vipi 
tathmini au changanua hizo zinavyo-fanyika.  

Misuguwano ya Miundo ya Demokrasia na Uchumi.

Ni kiasi cha miaka 30 tokea Tanzania kupata hicho kiitwacho "Soko-Huru  na Demokrasia ya vyama vingi ".
Kuanzishwa kw mfumo huu ni matokeo ya ushawishi mkubwa na nguvu za massive propaganda za nchi za 
magharibi katika vita vyao baridi dhidi ya ukoministi na nchi ambazo zilikuwa na siasa dhidi ya ubepari na 
ubeberu wa ulimwengu.Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na Mfumo wa Chama Kimoja nchini nayo ilikuwa 
inapigwa vita na maaduwi wa ndani na nje ya Tanzania . Kwa sababu ambazo hazikuweza kukwepeka na
usaliti ndani ya chama tawala viongoozi wetu kwa njama tofauti taifa likasakamizwa kwenye mfumo ule
uliobatizwa "Kila Kitu Rukhsa " mfumo ambao ndio uliengeza nafasi za ufisadi wa mali za taifa na kubomoa
hata silka na utamaduni mzima wa Watanzania na hat nchi za jirani.
 
Hivi karibuni palifanyika mkutano mjini Kigali huko Rwanda.Lengo la mkutno huo lilikuwa ni kujaili miundo 
na taratibu za Demokrasia na Uchumi katika nchi changa duniani .
Wajumbe kutoka nchi 47  za  Afrika na Asia walihudhuria katika mkutano na akashiriki kwenye michuao mikali 
ya itikadi hasa kwenye uchambuzi  wa "Democratic Models " zinazoigizwa-igizwa kwa U-Imla wa dola kubwa za 
Umagharibi kupitia chombo chao cha IMF.

Ushawishi huu wa nchi za Afrika kulazimishwa kuigiza "Democratic models" za Uingereza-Marekani au France
umeathiri sana nchi zetu.Wanaosukuma-sukuma itikadi za soko-huru na Uneo-liberali;walitudanganya hapo 
mwanzoni wakati wa awamu ya pili bila ya kuona aibu ya makosa yaliotendeka .Waliongia kwenye madaraka
ya awamu ya tatu ,nao wakatudanganya na hawa viongozi wa vyama tofauti vya upinzani ambao ni "makapi"
yaliyolelewa na kunufaika ki elimu,ki nafasi za kazi na ndio waliofisidi mali za taifa ,hivi sasa tokea 1992 mara
tu baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi wamo katika njama na mipango ya kudanganya Watanzania wa
pande zote mbili kwamba "Utawala wa Demokrasia Yao - utakuwa ni wa "haki kwa wote " kwenye mfumo huu
huu wa soko-huru la "Kila Kitu Rukhsa" na ni "Haki kwa wote ". Sasa  tujiulize ; patakuwa na tofauti gani baina
ya wa akina "kila kitu rukhsa " na hawa akina "haki kwa wote " ikiwa mtido na muundo uchumi na demokrasia 
itakuwa ni ya aina hii hii ya uliberali mambo leo ambao haujanufaisha wengi wa wananchi?

Siasa za Ulberali mambo leo imehalalisha,imeharakisha na kujadidisha njama za ufisadi wa mali za taifa.
Walio kwepa kidanganyifu Azimio la Arusha na kupata utajiri wa haraka-haraka wamezidi kuwa matajiri kuliko
hapo kabliya .Umasikini umezidi kutiya mizizi na kuwa mkubwa;umasikini ambao nao umezusha na kuzaa Ukatili
Utapeli-Ujangiri na Ujambazi.Wanasiasa wetu walifanya ushabiki wa kuigiza miundo ambayo si sambamba na
mazingara halisi ya nchi zetu,na ndio maana badala ya kuwepo Demokrasia tukaombolea Mockrasia. 

Vipi Tanzania  au Afrika kwa Ujumla itapata Demokrasia  ?
    
Suala hili ni sugu ,kwa sababu ya ukosefu uliojisheheni katika hulka na tabia za baadhi ya viongozi wa vyama vyote
khasa vile vya wanaotawala na vingi vya Upinzani .Itawezekanaje kupata Demokrasia wakati Uongozi wa vyama
unakuwa `dictated and decided ` na hao hao wanao-vimiliki vyama hivyo na sio kura za uhakika na za dhati zenye
uthabiti wa chaguo la wanachama. Ndio maana nikasem hii siyo Demokrasia bali ni dhihaka ya Mockrasia.

Vyama vya siasa takriba vyote vya upinzani vina-kelele-kelele za kuwaa na "ready made solutions" kwa matatizo
yote nchini ,lakini taratibu za kusuluhisha matatozo hayo hazitaweza kupatikana mpaka kila mmoja kati ya hao
viongozi wa upinzani washike madaraka ya Urais au Uwaziri Mkuu .
Zanzibar ina wananchi milioni moja na zaidi na idadi ya matatizo ni hiyo hiyo ya milioni na zaidi ya hapo ;sasa hebu
tujiulize Zainzibar with 1.3 million problem solvers ;solutions ya nani na rais gani ndie atakaye kuwa bora ambae
ataweza kutatuwa matatizo yoye milioni moja na zaidi katika nchi ? Tanzania Bara nao kwa idadi ya millioni 45 za
binaadam tatizo ni hilo hilo .

Nini cha kufanya ?

Inaajulikana kwamba asili 75% ni vijana wenye chini ya umri wa miaka 50 na hao ndio wengi wa wapiga kura
kote nchini ikiwa ni Visiwani au Bara Kwa hivyo ,inawabidi wasimame kidete wawaambie viongozi wote wa 
siasa -ikiwa ni wale wa chama tawala na au vya upinzani kwamba " You fooled us once,shaame on you;you fooled
us again and again ;elections after elections ,shame on us , us the youth ,us the people for possesing very short 
memories wasting our votes for nothing. Tunaunda chama chetu kwa vijana tu walio chini ya miaka 50. 
Na hii mizee iliyofanya kupiga  bwabwaja na porojo la siasa ndio kazi na njia pekee ya kula - hivi sasa waende
wakapumzike - tumechoka nao . 
 
Benn Haidari
Klintvägen 16 C 36
22100 Mariehamn
Åland
Suomi-Finland
Author of Modern Zanzibar Cuisine
Tel/Home: +358.18.13665
Mobile: +358.457.3424826

Share this :

Related Posts

0 Comments