[wanabidii] CHADEMA WASHIKWA KORODANI NA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Wednesday, July 16, 2014

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA INATISHAA.CHADEMA WAFYATA MKIA SASA KUITISHA UCHAGUZI NDANI YA CHAMA.
(MAKUNDI YAANZA KUJIPANGA UPYAA)

Baada ya msajili wa VYAMA vya siasa kuwataka chadema kuitisha uchaguzi ndani ya chama chao kwa mujibu wa katiba yao sasa chama hicho kimekubaliana na hoja hiyo ambayo kimsingi wanachama wengi na wajumbe wengi walikuwa wanasubiri hasaa kutokana na purukushani zao ndani ya chama.

Jana chama hichokupitia kwa katibu mkuu Dk slaa kimetangaza kufanyika kwa uchaguzi huwo.
ambae amedai utawapisha watu wote wenye nia ya kugombea nafasi yoyote na kudai utakuwa uhuru na haki,tujiulize kweli utakuwa huru ?

Wakati chama kikitangaza hayo tayari kuna minongono ya ule mgogoro kurudi upya tena baada kundi kubwa lenye nguvu ya kisiasa kuwa tofauti na uongozi uliopo kwa maslai ya kukiokoa chama.

Habari iliopo ni kuwa wajumbe wote karibu wa mkutano mkuu na wale wa baraza wanapingana na viongozi wakuu.

Hoja zao kubwa ni Mambo ya ufujwaji wa hela za chama na mwenendo wa ufanyaji kazi wa chama.
wajumbe hawa wamedai wanataka uchaguzi huru na haki itendeke vizuri.

Akiongea ktk ofisi ndogo iliopo mtaa wa togo kindoni mjumbe mmoja wa baraza kuu la uongozi kuwa tayari baadhi ya wajumbe wanasubiri kuja kusema maovu yote yaliopo ndani ya chama na hatimae kuwachagua viongozi wanaowataka.mjumbe huyo hajataka kujiweka wazi ametokea mkoa gani.

(Watu wanadai sasa vita ya uongozi ndani ya chadema yarejea upya Baada ya chama kutangaza kufanyika uchaguzi huwo.)

Kama mdau wa kisiasa kwa hali hiyo ya chadema kutangaza uchaguzi nini faida yake na Nini hasara yake ?
karibuni wadau.
Asante.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments