[wanabidii] UHAMIAJI WAMEONYESHA UWAZI KATIKA USAILI

Saturday, June 14, 2014
Ndugu zangu ,

Toka juzi nimeona watu kadhaa wakiponda hatua ya Idara ya uhamiaji kuita kwenye usaili watu zaidi ya alfu 1 wakati wanaotakiwa ni watu 70 tu .

Kuna jamaa wamechukulia hili kama ajenda ya kisiasa na kuanza kuhoji au kurushia vijembe vyama vingine vya kisiasa kusuatia kadhia hiyo .

Tunachopaswa kujua ni kwamba idara ya Uhamiaji ni Nyeti kama zilivyo idara nyingine za kiulinzi na usalama nchini , mchujo wake unahusisha vitu vingi sana kuliko ilivyo awali , sio elimu tu na afya tu kuna masuala ya uelewa wa vitu mbalimbali , historia yako ya nyuma , mahusiano yako na hata kwenye mafunzo na mazoezi kabla ya kuanza kazi rasmi .

Kwahiyo ukichukuwa watu hao alfu 1 au 2 , ukiwaweka kwenye mizani hiyo unaweza kupata hao 70 au usipate kabisa kutegemeana na vigezo vilivyowekwa na idara yenyewe .

Naipongeza idara kwa hatua yake ya kuwa wazi kwa kuita watu kwa mkupuo sehemu moja kwa ajili ya usaili , maana pale msailiwa anaangaliwa toka wakati anaingia uwanjani , atakavyowasiliana na wenzake na masuala mengine mengi , ndio tupo kwenye dunia hiyo ya kuangaliana kabla ya majukumu .

Tumeona operesheni ya kuondoa wahamiaji haramu ilivyoleta madudu mengi nchini mpaka kuundwa kamati na wengine kujiuzuru , hatupendi hiyo itokee tena ndio maana usaili unatakiwa uwe wa makini , wawazi na wenye viwango .

Tusipende kuponda na kudharau kila kitu haswa hivi vinavyohusu usalama wetu wenyewe .


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments