[wanabidii] POLISI WAPIGA WAUZA MAANDAZI MABOMU YA MACHOZI POSTA ,DAR

Monday, June 16, 2014
Abiria wengi wanaoshukia Posta mpya Jijini Dar es Salaam, wamejikuta wakilazimika kununua maji kukabiliana na mabomu ya machozi yaliyorushwa na polisi wakisaidiana na Mgambo wa Jiji. Sababu inasemekeana ni kuwafukuza akina mama wanaouza maandazi, vitumbua na mihogo kwenye hilo eneo. Wengine ambao hawakuwa wahusika katika operesheni hiyo ndio walioathiriwa zaidi, wanafunzi, wafanyakazi, madereva na makondacta kila mmoja anajua alivyoathirika. Nimeshangaa sana kuona polisi wanatumia mabomu kuondoa wauza vitumbua. Nchi yetu??? Nguvu hii ilihitajika hapa? Serikali yetu itapata lini akili??

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments