KESI YA KUPINGA UCHAGUZI SIMBA KUSIKILIZWA LEO
Na Happiness KatabaziMAHAKAMA Kuu Kanda Ya Dar es Salaam, leo itaanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na wanachama wa tatu wa Timu ya Soka ya Simba, ambao wanakomba mahakama hiyo itoe amri ya Muda ya Kuzuia kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Timu hiyo ambao umepangwa kufanyika Juni 29 Mwaka huu.
Akizungumza na Tanzania Daima Jana mchana, Wakili wa wanachama Hao, Revocatus Kuuli alisema uongozi wa Mahakama umempatia Jaji Augustine Mwarija kuisikiliza na inaanza kusikilizwa kusikilizwa Leo.
Endapo Jaji Mwarija atasikiliza Kesi hii Na.291/2014 Kama ilivyopangwa, itakuwa ni Mara yake ya pili kusikiliza Kesi ya aina hiyo. Mara ya Kwanza ilikuwa ni Mei 8 Mwaka 2010 ambapo Jaji Mwarija akiwa na wa Mahakama hiyo alitoa amri ya kubatirisha amri ya muda ya kuzuia uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba uliofanyika Mei 9 mwaka 2010.
Amri ya kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa simba iliyotenguliwa na jaji huyo ilitolewa Mei 6 mwaka 2010 na aliyekuwa Hakimu Mkazi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Amiceth Wambura ambapo Jaji Mwarija Alisema Amefikia uamuzi wa kutengua amri hiyo baada ya kubaini kuwepo Kwa dosari Katika amri ile ya Mahakama ya Kisutu.
Amri hiyo ilitolewa saa 1:10 jioni na Jaji Agustine Mwarija baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili zilizokuwa zinavutana katika kesi iliyokuwa imefunguliwa na Michael Wambura dhidi ya mwenyekiti wa klabu ya Simba, wa wakati huo, Hassan Dalali, kuruhusu uchaguzi huo kuingiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Juni 23 mwaka huu, wananchama Hao watatu kupitia Wakili wao Kuuli walifungua mahakamani hapo Maombi hayo madogo, Na.291/2014 Josephat Waryoba, Said Lly Monero na Hassan Hassan, ambao wanamshitaki Rais wa Timu ya Simba, Ismail Aden Rage na Bodi ya Udhamini ya Timu hiyo.
Kwa mujibu wa hati hiyo inayonyesha walalamikaji wana jumla ya Madai matatu ambayo dai la kwanza wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya kuwazuia wadaiwa kuitisha uchaguzi Mkuu uliofangwa kufanyika Juni 29 Mwaka huu.
Wakili Kuuli analitaja ombi la pili ni wanaomba jumla ya wanachama 66 waunganishwe Kwenye Kesi hiyo ili nao wawe walalamikaji dhidi ya wadaiwa kwasababu wadaiwa ambao Rage na Bodi ya Wadhamini wamevunja Katiba ya Simba , taratibu za uchaguzi na na maadili ya uchaguzi , kadi za uanachama za wanachama hao zimearibiwa.
Wakili Kuuli alidai kuwa mdaiwa wa kwanza Kamati ya Utendaji ya Simba walishindwa kuweka sawa Kamati ya Maadili ya simba Kama inavyotakiwa na Katiba ya Timu hiyo na Kanuni za uchaguzi za TFF.
Alidai Kwa vitendo hivyo wadaiwa hao wamevunja taratibu zote za uchaguzi na kwamba Hakuna Chombo Cha klabu ya Simba ambacho kimepewa madaraka ya kusimama a masuala ya rufaa ya Maadili ya wanachama wake na kwamba rufaa zote zote zinazohusu Maadili zinasimamiwa na mdaiwa wa pili(Bodi ya wadhamini ya simba), nakwasababu hiyo wanaiomba Mahakama hiyo itafsiri Hilo.
" Japo Kuwa maelekezo toka TFF kwenda mdaiwa wa kwanza (rage) ya
Yaliyomtaka Rage aweke sehemu ya Kamati ya Maadili , Rage alishindwa kutekeleza maelekezo hayo KWA Madai Kuwa robo Tatu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Timu hiyo , wanatuhumiwa KWA makosa ya utovu wa Maadili .
" Barua ya TTF kwenda KWA Rage ya Mei 29 Mwaka huu ,na barua ya Mwenyekiti wa Simbaya Juni 17 Mwaka huu ambayo alikuwa akimjibu Rais wa TFF, Jamal Malinzi ni ambazo tumeziambatanisha katika hati yetu ya madai kama vielelezo ili mahakama itoe tafsiri ya sheria " alidai wakili huyo.
Aidha walalamikaji hao wanadai Kuwa Kamati ya Uchaguzi ya Simba ipo kinyume na Katiba ya Timu ya Simba Kwani Kamati hiyo Ina baadhi ya wanachama ambao walioteuliwa Na Kamati ya Utendaji na waliondolewa na Rais wa Timu hiyo Katika Kamati hiyo kinyume Cha Sheria .
Pia wamedai Kuwa Kamati ya uchaguzi ya simba haina mamlaka ya Kamati ya Maadili ya kuwandoa baadhi ya wagombea Katika mchakato wa uchaguzi Mkuu Kwani Kamati ya uchaguzi wa kuwachuja wagombea pekee na suala la utovu wa Maadili na nidhamu ya mgombea jukumu Hilo limekabidhiwa Kwenye Kamati ya Maadili peke na siyo Kamati ya Uchaguzi .
"Kwa Sababu hiyo tunaimba Mahala hii itamke Kuwa utaratibu wote wa kuendesha uchaguzi ndani Timu ya Simba ni batiri kwasababu umekiuka Katiba ya Simba" Alidai Wakili Kuuli.
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Juni 25 Mwaka 2014.
Sent from my iPad
0 Comments