Ndugu,
Majira haya ya tamasha kubwa la fainali za Kombe la Dunia, ni wakati pia kwa ulimwengu wa soka kuwakumbuka vijana hawa wa Waafrika waliokufa kwenye ajali ya ndege wakitokea Lusaka, Zambia.
Wapenzi wengi wa soka tunakumbuka tulikuwa wapi wakati tulipofikiwa na habari hizo za majonzi makubwa. Ilikuwa ni april 27 mwaka 1993.
Vijana wale wa 'KK Eleven' walikuwa wakielekea Senegal kucheza me chi muhimu kuwania tiketi ya kucheza kombe la dunia kwa mwaka 1994.
Walipofika pwani ya Gabon, ndege ile ya jeshi ilianguka. Abiria wote 30 walipoteza maisha. Kikosi cha Zambia kinachoonekana pichani http://mjengwablog.com kilikuwa na wachezaji 18.
Aliyenusurika alikuwa nahodha Kalusha Bwalya anbaye alikuwa akichezea Ajax Amsterdam na alipanga kuungana na wenzake Dakar, Senegal.
Lakini kimsingi kizazi kizima cha soka ya zambia kilipotea akiwamo kocha mzalendo Godfrey Chitalu.
Kwa kuwapa pole, nchi ya Denmark ilitoa ofa kwa Zambia kupokea kikosi cha timu ya vijana ya zambia ambacho kilipiga kambi ya miezi kadhaa nchini Denmark kujipanga upya ili kuunda timu mpya ya taifa.
Dunia ya soka itawakumbuka daima vijana wale wa Zambia waliokufa wakipigania kuiletea heshima nchi yao na bara la Afrika.
Maggid Mjengwa.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments