[Mabadiliko] MWIGULU ANAPOGEUZA KIFO CHA MAMA ZITTO KUWA SIASA!!!!

Monday, June 02, 2014
Walio wengi wanaungana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe. Binafsi ninajua uchungu wa kufiwa na mama. Nilifiwa na mama mzazi Februari 17, 2010 katika hospitali wa Bugando kule Mwanza, tukamzika siku tatu baadaye kijijini kwetu Busaraga wilaya ya Butiama. Ninajua uchungu wa kufiwa na mama na ndio maana, ninatambua namna ambavyo Zitto, ndugu na jamaa zake hawahitaji jambo jingine lolote katika muda huu isipokuwa FARAJA.

Si Zitto pekee, ila kwa yeyote anayefiwa. FARAJA ni jambo lililo kuu.

Katikati ya ukweli huo, nimemsikia bungeni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) , Mwigulu Nchemba, akiikejeli Chadema kuhusu kifo cha Mama Zitto! Sikutegemea! Kweli kiongozi huyo amefikia ukomo wa ubinadamu hata kukiingiza kifo cha mama yetu bungeni, akitaka kukigeuza kuwa sehemu ya KUPIGA SIASA.

Binafsi utamaduni, hulka, mazoea na nia kama hiyo naviona kuwa miongoni mwa MAMBO MACHAFU yasiyopaswa kupuuzwa, kushangiliwa ama kuungwa mkono.

Ingawa kifo ni hitimisho la uhai duniani na mwanzo wa safari ya kuekelea kwa BABA, lakini ni sehemu inayoibua uchungu na simanzi pengine kuliko vyote.

Nawaombea Zitto, ndugu na jamaa zake wawe na nguvu na Mwenyezi Mungu awajalie faraja iliyo kuu katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa Mama mpebdwa.

Mashaka Mgeta

Share this :

Related Posts

0 Comments