[Mabadiliko] Je, Wajua? George Weah Ni Mwafrika Aliyepata Vyote Katika Soka, Kasoro Kucheza Fainali Za Kombe La Dunia...

Saturday, June 14, 2014


Ndugu zangu,

Huenda si wengi wenye kufahamu, kuwa George Weah ndiye mchezaji wa kwanza kutoka nchi ya Kiafrika kupata kutunukiwa tuzo ya Mwanasoka Bora Duniani. George Weah anatoka nchi ya Liberia.
Ilikuwa ni mwezi Desemba, mwaka 1995, ni pale FIFA ilipoitangazia dunia ya soka, kuwa George Weah amechaguliwa kwa kupigiwa kura kuwa mwanasoka bora wa dunia.

Na mwaka huo huo, George Weah akawa Mwanasoka Bora wa Ulaya, na haikuishia hapo, akatangazwa pia kuwa Mwanasoka Bora wa Afrika! Mwaka mmoja mataji matatu!

George Weah alianza kusakata kabumbu nchini mwake Liberia kabla ya kuhamia klabu cha Monaco, na baadae Paris Saint Germain. Mwaka 1995 akaenda kwenye klabu ya Milan na ndipo akafikia kilele cha mafanikio yake katika soka. Kwenye uwanja wa nyumbani wa San Siro wa timu ya Milan, George Weah alikuwa mfalme aliyependwa sana na wapenzi wa Milan.

Baadae, George Weah akaenda kuchezea Chelsea na Manchester City.

Pamoja na mafanikio makubwa katika soka, George Weah hakuwahi kushiriki kucheza fainali za Kombe la Dunia. Na bila shaka, kwa kusukumwa na hamu ya kuiona nchi yake ikiongozwa na mtu atakayeweza kuifanya itulie na kuondokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe na hata kucheza kombe la dunia, mwaka 2005, George Weah akaamua ' kucheza kandanda ya majukwaa ya siasa'. Alishiriki uchaguzi mkuu wa Liberia. Aligombea Urais wa Liberia, Huko akakutana na wenye kujua ' kucheza siasa'.

George Weah akagalagazwa na mwanamama Ellen Johnson - Sirleaf.

Maggid Mjengwa,
0754 678 252

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAMD-ye6pGhJKenSPZ62MHCZjQaaoYFsYC8pFnnv98VSRUxzu%2BQ%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments