[wanabidii] Wenye ulemavu waliotimuliwa Kariakoo wataka Serikali iwape mshahara

Monday, May 19, 2014
Watu wenye ulemavu waliotimuliwa kutoka Mtaa wa Kongo jijini Dar es Salaam waliandamana mwishoni mwa wiki hadi kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa huo wakidai malipo ya kiasi cha fedha, shilingi 400,000/= kila mwezi.

Watu hao waliofika hapo majira ya saa tatu asubuhi na kuwaacha na bumbuwazi wafanyakazi wa ofisi hizo, wamedai kufukuzwa kwao bila ya kuwapatia maeneo mbadala ya kufanyia shughuli zao za uchuuzi kumewasababisha wakose kipato cha kujikimu wao na familia zao.

Wakiongea na gazeti la The Guardian la Jumapili wamesema wameshindwa, mathalan, kulipia ada ya za shule kwa watoto wao na hivyo kuitaka Serikali ichukue jukumu la kuyaangalia maisha yao kwa kuwa ndiyo iliyowatimua wasifanye biashara wala kuwa ombaomba.

Mmoja wao aliilaumu Serikali kwa kuwatelekeza na kuwatumia tu kama mtaji wa kura nyakati za uchaguzi lakini huishia kuwasahau punde waingiapo madarakani, tofauti na nchi nyingine ambapo walemavu hupewa kipaumbele ili waweze kujitegemea.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments