[wanabidii] Watatu wauawa kwa bomu Mombasa

Saturday, May 03, 2014
Kwa mujibu wa taarifa bomu la mkono lilitupwa kwenye basi katika eneo la Mwembe Tayari ambalo hupendwa kutembelewa na watalii na kusababisha vifo hivyo na wengine kujeruhiwa.

Mlipuko mwingine umesikika katika hoteli moja eneo la mwambao wa bahari la Nyali. Hakuna taarifa zozote za vifo wala majeruhi.

Kenya imekuwa ikikumbwa na matukio ya mashambulio yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la kiislamu la Alshabaab la nchini Somalia.

Aidha nchi hiyo imekuwa katika tahadhari tangu mwezi Septemba mwaka jana ambapo wanamgambo wa Alshabaab walivamia kituo cha biashara cha Westgate kilichopo mji mkuu wa Nairobi na kuua watu wapatao 67.

Al Shabaab ni kundi ambalo lina uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda ambalo limeapa kulipiza kisasi kufuatia Kenya kutuma majeshi yake nchini Somalia mwaka 2011ambayo yameungana na yale ya Umoja wa Afrika AMISOM.

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/05/140503_mombasa_blast.shtml

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments