Asalamu alaikhum nduguzangu Wazanzibari wa Ndani na Nje ya Visiwa Vyetu Adhimu.
Hutuba ya Shekh KISHKI
MAKAMO wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, MaalimSeif Sharif Hamad, alikuwamiongoni mwa maelfu yaWaislamu walioshirikifaradhi kifaya ya kumzikaSheikh Ilunga HassanKapungu siku ya Jumatatuwiki hii.
Kama alivyosema Sheikh'Kishki' katika nasaha zake pale msikitini TIC, Magomeni Kichangani, Maalim Seif kashiriki maziko yale kama Muislamu. Alishiriki kumzika Muislamu mwenzake kama Uislamu unavyohimiza.'Kishki' akatumia fursa hiyo kuwazindua viongozi wengine wa kiserikali na wanasiasa kwamba,kuwa kwao madarakani hakuwaondolei wajibu wao wa kidini. Akawataka,wasione fahari tu kujitokeza kushiriki maziko yawana muziki, 'Bongo movies', na mambo kama hayo, lakini vyema zaidi waone fahari kujumuika na Waislamu wenzao katika maziko kama yale ya Sheikh Ilunga.
Katika muktadha huu,pamoja na kuchukuliwa kwamba Maalim kaja kama Muislamu, na si kama kiongozi wa kisiasa au kama Mzanzibari, lakini pengine ingekuwa vyema kutumia fursa hii kusema yale ambayo Sheikh Ilunga aliyasema mwaka 2011 kama nasaha zake kwa Maalim Seif na viongozi wenzake wa Zanzibar na Wazanzibari wote. Katika muhadhara wake mmoja kule Pemba, Sheikh Ilunga alisema kuwa kabari ya mfumo kristo imewakaba barabara Wazanzibari,hawafurukuti. Hata hivyo,pamoja na hali hiyo,Sheikh Ilunga aliwataka Wazanzibari kuto kukata tamaa, bali watumie fursa zilizopo kurejesha hadhi yao.
Fursa ya kwanza akasema ni wao kuwa Waislamu. Akawataka watizame kwanza hadhi ya Uislamu, ndio ifuatie nchi yao na dola yao. Alisema kuwa,Wazanzibari ni lazima watumie maridhiano ya kisiasa yaliyopo ili kuleta maridhiano ya Kiislamu. Kwamba amani iliyopo itumike kuimarisha udugu wa Kiislamu, watu wajitambue kwamba wao ni Waislamu kwanza kabla ya jambo jingine lolote. Ni Waislamu kabla ya CUF, Ni Waislamu kabla ya CCM na ni Waislamu kabla ya kuwepo Tanzania na Muungano wake. Akasema hilo linahitaji Da'wah ya kutosha na watu warejee katika Qur'an walonena kutafakari jinsi Mwenyezi Mungu anavyo waonya juu ya kuwafanya Mayahudi na Manasara kuwa marafiki na wasiri wao.
Akawakumbusha pia kuwa Qur'an imesema wazi kwamba chuki iliyofichwa na Manasara ndani ya vifua vyao ni kubwa mno kuliko wanayo idhihirisha na kwamba hawataridhia mpaka wawaritadishe Waislamu, japo wabakie Waislamu wa majina lakini makafiri kwa kauli, vitendo na maadili. Kufuatia kauli ya Bwana William Lukuvi Kanisani na Bungeni, bila shaka maneno haya ya Shekh Ilunga yanathibitika zaidi. Kwamba ipo chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Na hiyo namna pekee ya kukabiliana nayo, ni kujitizama kama Waislamu, kama Lukuvi na waliokuwa Kanisani pamoja naye walivyo jitizama kama Wakristo kutoa hofu yao dhidi ya Waislamu walio wengi Zanzibar.
Baada ya neema ya Uislamu, na fursa ya kuwepo maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa ( G.N.U), shekh Ilunga alitaja fursa nyingine kuwa ni mabadiliko ya katiba yanayokuja. Akasema, ni lazima fursa hiyo itumike vizuri kuhakikisha kuwa kichakakinachoficha mfumo kristokinapigwa moto. Na hiyo itafanyika kwakuwa na muungano wahaki ambapo pande mbili za Muungano, Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na haki sawa, sio huu wa serikali ya Tanganyika kujivika joho la Serikali ya Tanzania.
Shekh Ilunga alimalizia kwakuwapa changamoto viongozi wa serikali ya Zanzibar,Rais Ali Mohammed Shein,na Makamo wake wawili, Maalim Seif Sharif Hamad na Balozi Seif Ali Iddi kwamba wao wametoka katika migongo ya wazee wa Kiislamu na hivyo, hawawezi kukwepa jukumu la kuona hadhi ya Uislamu inarudi kama ilivyokuwa wakati wakilelewa na wazee wao. Kabla ya kutoa nasaha hizo, Sheikh Ilunga alisema kuwa mfumo wa Muungano uliopo umekuwa kama
kichaka unakojificha mfumo kristo kuiburura Zanzibar katika idhilali kwa kuipora nguvu zake za kisiasa na kiuchumi na kubwa zaidi kuhujumu Uislamu na Waislamu.
Aliyabainisha hayo katika kongamano lililofanyika katika eneo la Markazi Tabligh, Ole Kianga, Pemba Jumapili Oktoba 2011. Kongamano hilo lililohudhuriwa na maelfu ya Waislamu kutoka sehemu mbalimbali za Pemba, lilijadili hatari ya mfumo kristo kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Awali Sheikh Ilunga Hassan Kapungu alisema kuwa, inaweza kuwa jambo lisilo eleweka ukizungumzia mfumo kristo alisema japo kwa vile takriban viongozi wote waserikali na taasisi muhimu Zanzibar ni Waislamu, Wapemba na Waunguja. Hata hivyo akasema kuwa,ile kuwa inaitwa ni serikaliya Zanzibar haina maana kuwa Serikali hiyo ni serikali inayo ongoza dola kwani mamlaka yote ya kisiasa yapo katika serikali ya muungano.
Akifafanua alisema kuwa yapo mambo ambayo Wazanzibari wangeta kakufanya au kuamua kwa masilahi ya Nchi yao ya Zanzibar. Lakini hawawezi kuyafanya kwavile Muungano umewapora nguvu za kisiasa. Na kwamba, yale mamlaka ya kidola na kisiasa ya Zanzibar yalizikwa nakusomewa talakini siku ASP ilipoungana na TANU ambapo CCM ilishika hatamu na maamuzi yote muhimu kuwa yanafanyika Dodoma. Akitoa mfano alitaja uchaguzi mkuu ambapo jina linalopitishwa kugombea Urais laweza kuwa lile ambalo halikupata ridhaa ya Wazanzibari. Na hata kuondoka madarakani, kiongozi anaweza kuondolewa bila ya Wazanzibari wenyewe waliompigia kura au vyombo vyao vya uwakilishi kama Baraza la Wawakilishi kuhusishwa. Akatajwa mfano wa Mzee Aboud Jumbe aliyekwenda mkutanoni Dodoma akiwa Rais akarudi Urais akiwa ameuacha Dodoma. Sheikh Ilunga kwa kutoamfano huo alisema kuwa Alhaj Aboud Jumbe, yalimfika kwasababu alihoji Muungano nakuhoji kwenyewe si kutaka kuuvunja, bali kutaka uwe wa haki.
"Yalimfika." "Kwa nini?"
"Kwa nini imefanywa kuwa mwiko kuhoji Muungano?" Alisema na kuhoji Shekh Ilunga. Kabla ya kutoa jawabu, Sheikh Ilunga alirejea pia hali ilivyokuwa wakati wa Mzee Abeid Aman Karume ambaye alishaonesha kuwa koti la Muungano linambana, lakini mauti yakamfika muda mfupi kabla ya kutimiza nia yake ya kulivua. Aligusia pia yaliyomfika Maalim Seif Sharif Hamad, hata hivyo hakutaka kufafanua bali akawataka Wazanzibari wenyewe wamuulize Maalim nini kilimkuta na kwa nini. Katika kukamilisha hoja yake akasema kuwa Muungano umefanywa jambo nyeti na mwiko kujadiliwa kwa sababu ndio uchochoro na kichaka mfumo kristo unakopitia kuiua Zanzibar na kuuwa Uislamu.
Katika hali hiyo akasema kuwa, Wazanzibari watakuwa wakiwalaumu na pengine hata kuwachukia bure viongozi wao, lakini nao wanashindwa kufanya yanayotakiwa na Wazanzibari kwasababu inabidi kwanza watizame Dodoma inasema nini. Kwa maana kuwa jambo kama halijapata ridhaa yamfumo Kristo, haliwezi kuwa kama ambavyo haikuweza Zanzibar kujiunga na OIC na hivi sasa Tanzania haiwezi kujiunga na jumuiya hiyo kwasababu Maaskofu hawataki, mfumo kristo hautaki. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernad Membe aliliambia rasmi Bunge kuwa serikali haioni tatizo Tanzania kujiunga na OIC, lakini ghafla msimamo ukabadilika baada ya kuitwa na Kardinali Pengo.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments