[wanabidii] UJUMBE KWA WACHUNGAJI, MAPADRI NA WAKRISTO

Thursday, May 15, 2014


Bwana Mungu asema" Nataka toba ya kitaifa ya kanisa, maombolezo na vilio" 

Ulipokelewa na Dkt. Augostino Maquengo
 
Bwana alinitembelea asubuhi mara tu nilipofika ofisini. Niliuhisi uwepo wake kisha mkono ukanijia juu ya mabega yangu. Nami nilihisi moto juu yangu na nikaisikia sauti ya Bwana ikiniongelesha ikisema: " Yaandike haya na uwaambie." Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenyezi Mungu kwa wachungaji, wainjilisti, mapadri na watumishi wengine:  "Ghadhabu yangu itawamaliza" Nanyi hamtanyakuliwa, kwani mmeziacha njia zangu na kuwafanya kondoo wangu mali yenu binafsi na chanzo cha utajiri wenu.
 
Kwa hiyo Bwana  asema, sitawanyakua wachungaji hawa, wanjilisti na watumishi wangu waliopenda mafanikio na kunyakuliwa, badala ya ujumbe wa toba, kubadilika, na kuja kwangu ambako kuko karibu. Kanisa wanalolisema kuwa langu, limekuwa ukumbi wa starehe likiongozwa na wachungaji, mapadri na mashemasi wa kanisa. Wanakula na kunywa na kusherehekea nyumbani mwangu na mbele yangu pasipo kuogopa, kutetemeka au kuniheshimu. 
 
Oh, utukufu wangu umeondoka makanisani mwao na uwepo wangu uliondoka kitambo kutoka makanisani mwao. Wao hawatanyakuliwa wasiponililia mimi Mungu wao kwa uchungu katika toba. Watumishi wangu wamepotoshwa na dunia nao sasa wanafanya mipango ya kuziingiza njia za kidunia makanisani.
 
Wao husherehekea siku ya wapendanao makanisani na pia husherehekea siku ya kimataifa ya waongo makanisani, nao hawasemi katika siku ya kuomboleza, leo ni siku ya majonzi nasi basi tuvalie mavazi meusi. Wote wamepotoshwa. Wachungaji, wainjilisti na mapadri wametabiri nyakati za mafanikio, nyakati za kukombolewa na kufanikiwa wakati hali inakuja humu ulimwenguni ya misiba na mateso makubwa, na kuharibiwa kwa ulimwengu. Watumishi wangu hawanisikii kamwe.
 
Wamejipotosha na dunia na hata wameziacha njia zangu.Wao hawanitafuti katika maombi, kufunga na kulitafakari neno langu. Wao hufunga na kuomba ili kuniomba vipawa vya kuponya, miujiza na kutabiri kwa manufaa yao wenyewe. Na hata wao husema: Nitatayarisha ujumbe wa kuhubiri. Nitatayarisha mkutano. Mimi nina shughuli nyingi ya kuwapa ushauri nasaha  waumini.
Lazima niwatunze waumini, nao hawana wakati kwa ajili yangu, Mimi, ambaye ndiye mmiliki wa kondoo hawa. Hawa wachungaji hawatanyakuliwa asema Bwana wa Majeshi. Ikiwa mnaniogopa mimi, basi zirarueni nguo zenu, nyoyo zenu na hata akili zenu kwa machozi na kutubu. Nataka toba ya kitaifa ya kanisa, maombolezo na vilio.
 
Mjivishe mavazi ya magunia na mlie kwa toba la sivyo nyinyi hamtakuja kwangu mbinguni. Kondoo wangu wanakula chakula kilichooza, kilichologwa  kutokana na jumbe za watumishi wangu na hawa wachungaji.
 
Wanawekeza kwa ajili ya siku za usoni kwa miradi ya ujenzi makanisani nao hawafahamu kwamba hii miradi yote itakatizwa na maangamizo na majanga ya ghafla. Baada ya kuliokoa kanisa langu kutoka humu ulimwenguni, hii miradi yote ya ujenzi itageuzwa kuwa bure. Ni uwekezaji ambao hautazaa chochote. Badala yake yafaa muwekeze katika kulihubiri neno lililio hai, lisilo ghoshiwa. Hubirini badala yake, kufanikiwa kwa nafsi na roho kupitia kwa toba na uzima wa milele.
 
Bwana asema hivi, nalipenda sana kanisa langu,ambalo hunitafuta kila siku na huliogopa jina langu takatifu!! Wakati umekwisha. Wakati umefikia tamati. Saa yaja sasa hivi, nitakapo linyakua kanisa langu.Mara tu baada ya tukio hilo, majanga, misiba, na mateso ya kutisha ambayo hayajawahi kutokea humu duniani, yataangamiza maisha mengi.
 
Wakati adui yangu atakapochukua hatamu, hapatakuwa na toba tena, wala wakati wa kunitafuta, kwani Mimi sitayajibu maombi yoyote, neema itakuwa imeondolewa na Roho wangu Mtakatifu hatakuwa ulimwenguni. Adui atachukua hatamu nanyi mtasaga meno yenu na kupiga mayowe mioyoni mwenu kwa mateso na kuvunjika.
 
Zivunjeni nyoyo zenu sasa na mzifanye zimwage damu ya toba, zirarueni nyoyo zenu kwa toba katika sekunde za mwisho za wakati uliosalia, la sivyo ghadhabu ya kutisha iwapate. Lakini watu hawa wana roho ya kuasi, nao wameasi na kwenda zao.
 
"Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche Bwana, Mungu wetu, aletaye mvua; mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea juma za mavuno zilizoamriwa. Maovu yenu yamegeuza haya, na dhambi zenu zimewazuilia mema msiyapate. Maana katika watu wangu wameonekana watu waovu; huotea kama vile watu wategao mtego; hutega mtego, na hunasa watu. Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali. Wamewanda sana, wang'aa; naam, wamepita kiasi kwa matendo maovu; hawatetei madai ya yatima, ili wapate kufanikiwa; wala hawa hawaamui haki ya mhitaji". (Yer.5:24-28)
 
Nyinyi hamtanyakuliwa asema Bwana, isipokuwa mbadilishe mienendo yenu na kutubu. Mimi sitawanyakua wale walio oana na televisheni, sinema na burudani ambazo zimechukua muda wenu mwingi, nanyi hamna wakati kwangu mimi Mungu na neno langu.
 
Mimi sitawanyakua wakristo waendao kanisani jumapili tu, ili kuituliza ghadhabu yangu juu ya maisha yao, nao wanadhani kwamba Mimi Mungu sioni wala kuyafahamu yale wafanyayo. Jumapili, wao huenda tu makanisani kujionyesha nguo zao nzuri na kupiga gumzo na marafiki wao.
 
Nyumba yangu imekua mtandao wa kijamii .Mimi Yesu Kristo, Bwana wenu sitawanyakua wale wanaoutumia muda wao mwingi kuitazama televisheni au katika kuvisoma vitabu vya riwaya na mambo mengine.
 
Kwa sababu wamezigeuza riwaya hizo pamoja na mafunzo ya kisayansi kuwa washauri wao, badala ya kuwa na Roho Mtakatifu kama rafiki wao wa kweli tena bora. Muumini yeyote aliyesahau kumtafuta Roho wangu Mtakatifu na kuifanya  televisheni na itikadi zingine za kipepo kuwa marafiki wake wa dhati badala ya neno langu ataachwa nyuma kukumbana na mpinga Kristo na alama ya mnyama muovu.
 
Kwa msaada zaidi kuhusu TOBA - (REPENTANCE REVOLUTION) tembelea tovuti hii;
        
                             www.aggressivechristianity.net 



Share this :

Related Posts

0 Comments