JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI KUHUSU ZAWADI KWA WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI KATIKA MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013
Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Elimu kilifanyika tarehe 10 Mei, 2014 katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambapo tuzo mbalimbali zilitolewa zikiwemo za fedha na zile zisizo za fedha kwa makundi tofauti tofauti.
Tuzo ya fedha taslimu ilitolewa kwa wanafunzi 30 waliofanya vizuri katika mtihani wa mwaka 2013 ambapo wanafunzi watano bora wasichana na watano bora wavulana waliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kumaliza Elimu ya Msingi walipata shilingi 125,000/=, Wanafunzi watano bora wasichana na watano bora wavulana waliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kumaliza Elimu ya Sekondari Kidato cha Nne walipata shilingi 250,000/= na Wanafunzi watano bora wasichana na watano bora wavulana waliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kumaliza Elimu ya Sekondari Kidato cha Sita walipata shilingi 500,000/=.
Fedha hizi zilitolewa na serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja na Ubalozi wa Jamhuri ya Watu wa China na zilitolewa kama fedha taslimu.
Aidha, fedha nyingine taslimu iliyotolewa ilikuwa ni Hundi ya Shilingi 3,000,000/= kwa walimu wa shule 60 zilizoongeza ufaulu katika mtihani wa mwaka 2013.
Pamoja na fedha taslimu za shilingi 250,000/= wanafunzi 10 wa Kidato cha Nne walipewa vocha za thamani ya shilingi 500,000/= kwa ajili ya kununulia vitabu vya kiada na ziada.
Aidha, Wizara imeamua kuwakabidhi wanafunzi 10 wa Kidato cha Nne fedha taslimu Sh. 500,000/= badala ya vocha ili wanunue vitabu wao wenyewe. Hii ni kwasababu wanafunzi hawa wanaweza kujiunga na Kidato cha Tano katika tahasusi (combination) mbalimbali na ni vyema wakanunua vitabu kulingana na tahasusi zao.
Katika kutoa zawadi hizo yamejitokeza mapungufu kadhaa ambayo yalisababisha usumbufu kwa baadhi ya wanafunzi na wazazi wao waliofika Dodoma kupokea zawadi hizo.
Wizara inaomba radhi kwa wanafunzi na wazazi hao kutokana na usumbufu uliojitokeza. Aidha, matatizo yaliyojitokeza yameshatatuliwa.
Prof. Sifuni E. Mchome
KATIBU MKUU
26/5/2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments