[wanabidii] Taarifa kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani 2014

Saturday, May 03, 2014
TANZANIA MIDWIVES ASSOCIATION (TAMA

Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA) kitaadhimisha siku ya Wakunga Duniani
(International Day of Midwives hapa nchini kwa siku mbili kuanzia tarehe 4 hadi 5/2015.

Siku ya Wakunga Duniani huadhimishwa duniani kote tarehe tano mwezi wa tano ya kila mwaka. Madhumuni ya Maadhimisho hayo ni kuhamasisha Wadau mbalimbali pamoja na Jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa wakunga na shughuli wanazozifanya katika kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi pamoja na vifo vya watoto wachanga na wenye umri chini ya miaka mitano.

Kauli Mbiu ya Mwaka huu (2014) ni "Wakunga Wataalam Wanahitajika Duniani kwa
 
wingi sasa kuliko siku zote." (The World Needs Midwives Today Than Ever)

Hii inalenga katika kuhakikisha kuwa huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto zinatolewa na Wakunga wenye utalaam kwa kufuata miongozo na viwango vilivyowekwa ili
kuchangia katika kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia namba 3,4, 5 na 6.

Tanzania ni mmojawapo ya nchi zenye uhaba wa watao huduma wenye ujuzi
hususani Wakunga katika ngazi ya zahanati na vituo vya afya ambako ndiko wakinana mama wengi wanapata huduma ya wakiwa wajawazito, kujifungua na baada ya kujifungua.

Katika kuadhimisha siku hiyo, Wakunga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
watafanya shughili tatu ambazo ni:

1. Kongamano la kisayansi kwa siku moja tarehe 4/5/2014 ambapo watajadili
mada na shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wakunga.

Mahali : Hospitali ya Taifa ya Muhimhili Jengo la New OPD Chumba no 60, linaloangaliana na Wadi ya Wazazi

Mgeni Rasmi: Mheshimiwa Dkt. Seif S Rashidi (MB) Waziri wa Afya na Ustawi Wa Jamii

2. Kutoa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika viwanja vya Mnazimmoja kwa
akina mama, watoto , vijana na wanaume kwa siku mbili 4/hadi 5/2014. Huduma
zitakazotolewa ni:

 Uzazi wa mpango,
 Chanjo kwa watoto
 Ushauri na upimaji wa hiari wa virus vya UKIMWI,
 Uchunguzi wa saratani ya matiti na kizazi kwa akina mama
 Utoaji wa hiari wa damu.
 Elimu na ushauri kuhusu hudma ya Afya ya Uzazi na Mtoto
 Wanaume watapata sindano ya Pepopunda ( tetanus)

Huduma zitakazotolewa ni bure hakuna malipo.

3. Kufanya mandamano kutoka makao makuu ya Wizara ya Afya hadi Viwanja vya
Mnazimmoja siku ya kilele tarehe 5/5/2014. Maandamano yataongozwa na Brass
band ya JKT Mgulani.

 Mgeni Rasmi ni: Mheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mke wa Mh. Dkt. Jakaya
 Mrisho Kikwete Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa heshima na taadhima Chama kinaomba vyombo vya habari kutusaidia kutoa
taarifa kwa Wananchi.

TANZANIA MIDWIVES ASSOCIATION (TAMA)
SLP 65524
Dar es Salaam Tanzania

E-Mail: seolesh@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments