[wanabidii] HARUSI YA MH. VICKY KAMATA ILIYOKUWA IFANYIKE LEO KWISHNEI, MUME ATOROKA NA PESA ZA HARUSI

Sunday, May 25, 2014

Staa wa Bongo Fleva na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) anayewakilisha Vijana Mkoa wa Geita, Vicky Pascal Kamata akiwa na mchumba wake Charles Pai. 

kwamba ile harusi ya the Century iliyokuwa ifanyike leo Kempisk Hotel baina ya Mbunge Maarufu wa Viti Maalum CCM Mh. Vicky Kamata imepiga mwamba kutokana na ukweli kujulikana dakika ya mwisho jana kwamba Mchumba wake Mheshimiwa Mbunge ni Tapeli wa ajabu hapa nchini amabae amekuwa akiwadanganya sana kina dada wenye utajiri na kwamba Mh. Vicky Kamata anakuwa ni Mbebez wa tatu kutapeliwa na Mchumba huyu pichani. 

Ripoti inasema kwamba Juzi Mke wa kweli wa Mchumba huyo alijitokeza na hati zake Kanisani Catholic kwa Wachungaji waliomfahamisha Mchumba kwamba hakutakuwa na tendo la kufunga Ndoa Kanisani ndipo Mchumba huyo bwana Charles akatimka na jumla ya pesa za mchango wa harusi hiyo Shillingi Millioni 40. Jumla zilikuwa zimeshachangwa Shillingi Millioni 100, tayari USD $ 15,000 zilikuwa zimeshalipiwa kwa ajili ya Ukumbi wa Kempisk Hotel, tayari wageni waalikwa toka Geita walioshiriki kumchagua Mbunge huyo walishafika Dar wapo hapa, na cha kutisha zaidi ni kwamba Mheshimiwa Mbunge toka jana asubuhi ameshindwa kabisa kumpata mchumba huyo kwenye simu zake zote zimezimwa hazipatikani kabisa. Inasemekana baadhi ya Wabunge waliomchangia kwa kiwango kikubwa sana wameanza kulalamika kwa pembeni.

http://www.mtizamohuru.co.tz/aibu-ya-mwaka-harusi-ya-mh-vicky-kamata-iliyokuwa-ifanyike-leo-kwishnei-mume-atoroka-na-pesa-za-harusi/

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments