THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wazee wa Baraza la Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wamempongeza na kumshukuru
Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ufafanuzi na kuunga mkono hotuba yake kwa Bunge la Katiba
aliyoitoa tarehe 21 Machi, Mjini Dodoma.
Wazee hao wamefika Ikulu ya Dar es Salaam leo jioni , tarehe 9 Aprili,2014 na kuelezea
furaha yao kwa Rais Kikwete.
"Wazee wote tunakushukuru, tumefurahishwa sana na Hotuba ile kwani umetoa ufafanuzi
wa mambo mengi, kwa hivyo tumefika hapa kukufahamisha kuwa tumefurahishwa sana,
tuko pamoja nawe kwa hali ya aina yeyote " wamesema na kumueleza Rais kuwa wanayo
mabaraza katika Wilaya, Mikoa, Kata na hata Mashina.
"Tumefurahi sana , hotuba hii imetufungua na tumefunguka hivyo tunakuunga
mkono na tuko nawe katika hoja ya Serikali mbili kama ilivyo katika Chama Chetu." Wazee
hao waliongozwa na Bi. Khadija Jabir Mohammed ambaye ndiye kiongozi wao na Bw. Waziri
Mbwana Ali Katibu wa Wazee. Wazee wengine waliofika Ikulu ni Bw. Juma Ame Juma, Bw.
Mohammed Khamis Haji, Bw. Juma Khamis Khamis na Bw. Tabib Omar Makungu. Wengine
ni Alchui Khamis Alchui, Bw. Abdallah Rashid Abdalla na Bw. Haji Machano Haji.
Rais amewashukuru Wazee hao kwa kumtia moyo kwa kufika Ikulu kuelezea hisia zao ambapo
Rais amewaeleza Wazee hao kuwa takwimu zote alizotumia katika Hotuba yake amezitoa
kwenye ripoti ya Tume ya Jaji Warioba na kwamba hata maswali aliyokuwa akiuliza, alikuwa
akiyauliza kwa nia ya kuyatafutia majibu na majawabu ya misingi kama yalivyoandikwa kwenye
rasimu ya Tume.
"Takwimu zote nimetoa kwenye taarifa ya Tume, Maswali niliyouliza nimeyatoa kwenye
taarifa, pia kuna mambo ya uandishi ambayo hayakuwa yameandikwa sawasawa hivyo nina
wajibu wa kutoa tahadhari kwa wajumbe wa tume ili kuwa na uhakika wa dhana na tafsiri
zilizomo kwenye rasimu ya Tume" Rais Kikwete amefafanua zaidi.
Mwisho!
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu – Dar es Salaam.
9 Aprili, 2014
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments