[wanabidii] WASWAHILI NA MAMBO YA KISHIRIKINA

Tuesday, April 22, 2014
Ndugu zangu ,

Leo nimerudi toka safari yangu ya mbali kidogo , nilitakiwa kwenda sehemu nyingine hapa nchini leo hii lakini safari imengoja kidogo ila nimejionea vituko toka asubuhi .

KUDONGOKA KWA KIZEE UBUNGO 
Leo asubuhi wakati Natoka uwanja wa ndege kuna bibi kizee Fulani alidondoka karibu na mataa ya ubongo , kwa kile kishindo watu walifukuzana , kugeuka kumbe ni bibi kizee wakataka kuanza kumpiga bahati nzuri kulikuwa na askari wa JW aliyeingilia kati na kumwondoa eneo lile kumpeleka kituo cha urafiki lakini kwa miguu .

MREMBO KUPASUA NAZI KATIKATI YA MATAA , SAYANSI
Jioni hii wakati narudi zangu toka sehemu tukiwa kwenye foleni mbele yetu kulikuwa na bajaj.

Askari alivyoruhusu magari kuondoka tu , jamaa wa Bajaji akaenda katikati ya mataa mara akatokea mdada kwenye bajaj akapasua Nazi pale katikati ya barabara  trafiki aliyekuwa pembeni aliduwaa watu wakashangaa tu jamaa akaondoa bajaj yake kwa mwendo wa kasi akaingia maeneo ya sayansi akapotelea huko .
Hayo mambo 2 hapo juu nilikuwa nayasikia kwenye hadithi na wakati mwingine kuona kwenye picha lakini leo nimeshuhuduia live .

Wazazi wanatwambia Mwanangu kua unayone , leo nimeyaona .


--

Yona Fares Maro

Institut d'études de sécurité - SA


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments