Vurugu kubwa zimetokea usiku wa kuamkia leo baada maaskari polisi wa nchi ya Uganda kuingia bila taarifa ndani ya Tanzania kukamata wanaodaiwa kuwa wezi wa pikipiki. Maaskari hao walioingia na gari ya kiraia ktk kukamata waliwapiga watu wawili risasi na mmoja akakimbilia kujisalimisha kituo cha polisi cha Tanzania.
Wananchi wa upande wa Tanzania baada ya kujua kwamba wanaopiga risasi siyo watanzania walikusanyika na kutaka kuwaua ndipo walipokimbilia kituo cha polisi Tanzania. Wanachi zaidi ya 1000 walikusanyika usiku huo na kuvamia kituo cha polisi, lakini waliingia magari zaidi y 6 ya FFu toka Bukoba na kutawanya umati huo.
Mpaka sasa haijulikani gari hilo la Uganda na maaskari wake wako wapi. Tetesi zilizopo ni kuwa wamepelekwa Bukoba na nyingine zinasema walifanikiwa kutoroka ktk vurugu usiku huo.
Updates:
Taarifa za uhakika ni kwamba maaskari wa Uganda watano na gari lao walifanikwa kutoroka kwa njia za kimafia ila askari mmoja tu aliyejisalimisha mwenyewe akiwa na bunduki aina ya SMG na risasi 18 baada ya kuachwa na wenzake. Askari huyo anashikiliwa na jeshi la polisi mjini Bukoba!
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/635808-vurugu-zatifuka-mutukula-baada-ya-askari-wa-uganda-kuvamia-tanzania.html
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments