[wanabidii] VITA DHIDI YA UGAIDI: ANAYEWINDWA NI MUISLAMU!

Friday, April 04, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
VITA DHIDI YA UGAIDI: ANAYEWINDWA NI MUISLAMU!

Harakati ya Kiislamu Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki imehuzunishwa sana na mauaji ya Sheikh Abubakar Sharif,maarufu 'Makaburi' na mwanzake kwa jina la Hafidh Bahero.Tunalaani vikali mauaji haya ya kinyama yalioashiria unyama wa majangili hao. Twamuomba MwenyeziMungu aipe subra familia ya marehemu hawa na awalaze ndugu Abubakar na Haafidh mahala pema peponi. Fauka ya haya tungependa kutaja yafuatwayo:

Mauaji haya ya ndugu zetu hawa Makaburi na kabla yake mauaji ya masheikh wengine yanaashiria si tu uoga wa majangili hao bali nia yao mbovu ya kuwamaliza Waislamu na kuwanyamazisha wahubiri wa Kiislamu kutoulingania Uislamu kwa sura yake kamili ya kimfumo.

Mauaji haya yamefanya jamii ya Kiislamu ikose imani na vyombo vya usalama bali kuviona kuwa vinawajua wanaowauwa Waislamu. Twasema hivi kwa sababu kila wahubiri wa Kiislamu wanapouwawa polisi hudai kuwa haina habari juu ya mauaji haya na ati kuomba raia waje mbele yao kutoa ushahidi! Swali tunalouliza ni mbona katika mauaji yaliyotokea Likoni serikali mbio ilianzisha operesheni ya kuwasaka 'unkown assailants' na muda mchache ikatangazwa kuwa tayari washambulizi hao wameuwawa na polisi?? Na je mbona hatukusikia mwito wa kuwataka raia waje kutoa habari juu ya walioshambulia kanisa huko Likoni?

Kwa kuwa Sheikh Makaburi tayari alikuwa ameorodheshwa na Marekani katika orodha ya 'magaidi', basi moja kwa moja mauaji haya yana mahusiano makubwa na 'vita dhidi ya ugaidi'. Mara nyingi sisi husema kuwa vita hivi vinalenga kuwaangamiza Waislamu na Uislamu. Na sio siri tena kuwa kumejengwa rai kwa umma jumla (public opinion) kwamba Waislamu ni watu wenye itikadi kali, magaidi na wana siasa kali. Misemo ambayo Amerika peke yake ndiye anayeifasiri na kuipa maana anayoyataka yeye. Swali ni je: Ni nani anayepaswa kupachikwa misemo yote hii (magaidi, siasa kali, itikadi kali nk) kama si Amerika serikali ya kibepari inayotumia mabavu kueneza mfumo wake mchafu wa kibepari kama anavyofanya katika ulimwengu wa Kiislamu anavyotumia mauaji hayo kama njia ya kulazimisha fikra zake huku ikijiita kuwa ni mkombozi? Na hapa Afrika mara ngapi Wamagharibi huwafokea viongozi wa Kiafrika na kuwatishia kukata misaada ati kwa kuwa wanapiga vita fikra chafu za kimagharibi kama vile ndoa za jinsia moja. Je haya yote sio misimamo mikali na itikadi kali ikiwa kweli misemo hii ina chembe chembe za ukweli? Vipi nyinyi mnahukumu?

Shabani Mwalimu
Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments