[wanabidii] UKUMBUSHO KWA WANA CHADEMA DHIDI YA ZILIZO KUWA HARAKATI ZA KI HAINI

Wednesday, April 09, 2014
Leo tarehe 8/4/2014 katika historia

Nilifikri kwa mda kuyasema haya

Haya ntakayo yasema na huenda yasiwafrahishe nyote au baadhi yenu ,hasa wale wasio penda kukosolewa na kuamini katika kukosea

Unaweza kuniamini mimi ninapo sema ukweli haupendwi kwa watu walio wengi kuusikia.Na kuusema ukweli kumewagharimu watu wengi ikiwa katika siasa umewagharimu baadhi kupoptweza maisha na wengine " salama' yao kufukuzwa uanachama

Mimi sitapoteza uanachama kama wengine kwa sababu kadi ya uanachama na uanachama wangu naumiliki mimi

Utangulizi Mimi kwa jina na sifa ni kijana kama walivyo vijana wengine wan chi hii

Kama ulivyo ushwishi mwingi kwa sasa hivi vijana wengi kujiunga katika siasa nchini

Mwaka 2006 ,nilivutiwa na mfumo wa vyama vingi nchini.Na hivyo mapenzi yakanifanya nifungue mlango rasimi kwa kuvitizama vyama hivi kwa udadis mkubwa

Mwaka 2008 nilivutiwa zaidi na zilizo kuwa harakati za chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mwaka 2009 mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa 2010 nikiwa chuoni nikajiunga rasimi na CHADEMA ilivyo kwa Mh Leama na Mh Peter Msigwa ambao tunaweza kuwa na historia inayo fanana

Leo sio dhumunio kuu kuelezea historia hii,nikielewa wapo walio na historia ndefu sana zaidi ya umri wa mtu mzima sasa katika mfumo huu

Leo nimesimama hapa katika maono na harakati zilizo zimwa za Mh,Dr.Kitila Mkumbo,Mh.Samsoni Mwigamba na Mh.Zitto Kabwe

Ikiwa ni harakati ni harakati au maono yaliyo wapelekea wao kufukuzwa uanachama na ahadi za viongozi wa Chama baada ya hapo

Nimetanguliza hapo awali kwa kusema maoni haya huenda yasiwapendezeeni baadhi yetu kwa sababu hapo nyuma yalishapingwa

Japo nasema yalipingwa kwa sababu yalionekana ni ya ki "uhaini au mapinduzi nyuma ya uongozi harali lakini mukutadha wenyewe haukupewa mda kutafsriliwa kwa zama na nyakati

Na basi kichwa cha mada yangu kiwa :"UKUMBUSHO KWA WANA CHADEMA DHIDI YA ZILIZO KUWA HARAKATI ZA KI HAINI ZA Dr.KITILA MKUMBO,ZITTO ZUBERI NA SAMASONI MWIGAMBA'

Neno ukumbusho linabaki na maana ile ile likiwa lina beba kukumbusha
Nimeona niwakumbushe ili tujiweka sawa katika historian a tujiweka sawa kwa nyakati chama chetu kilicho nazo

Haya ndo yaliyo kuwa mawazo ya wengi ambayo hata mimi nilikubaliana nayo,mtakumbuka mara baada ya kukamatawa kwa ulio kuwa walaka wa Mh.Zitto na wenzake mazingira yalitafsriwa kama ni wa haini na walitaka kuafanya mapinduzi ya uongozi kwa njia harali za kiharamia na za kimapinduzi huku zikizika mfumo harali wa kusubiri uchaguzi harali wa kidemokrasia na kutumia ushawishi wa kawaida kwa wapiga kura na wakapata kuchaguliwa kiharali,na hivyo kama wangelifanikiwa wapo ambao wasingelewa mbinu zilizo wafikisha hapo

Na hivyo ilikuwa ni wasiwsi juu ya hilo hasa na hivyo kupelekea kuhisi kama ingekuja kujulikana badae ingeleta mpasuko ndani ya chama

Lakini kama mtakubuka vizuri wengi walio bahatika kuusoma ule waraka,karibia wote warikubaliana na watunga waraka ule nay ale yote yaliyo kuwa ndani ya walaka ule wakidai ni kweli waraka ulikuwa ukitoa na kubainisha mapungufu makubwa ambayo kwa sasa chama kilipaswa kukabiliana nayo.Na hivyo ukonekana kama ulikuwa mpango haramu ulio kuwa na njia sahihi kwa chama katika kukifikisha mbali kwenye mafaniko zaidi

Na leo tunaweza kuona mara baada ya mbwebwe nyingi za chama na wananchama za kuuzima uhaini na kusahau njia nzuri iliyo kuwa imebebwa na uhaini huo leo chama kimebaki katika giza tororo

Ni hivyo wale tulio kubalina na kuiona ile njia iliyo kuwa imebebwa na uhaini ule kama ilivyo kuwa hapo mwanzo kuwa ndio njia nzuri ya kukifikisha chama sehemu nzuri zaidi muamkeni na kuitizama tena

Na dhamira yenyewe ilikuwa ni kuubadilisha uongozi wa juu wa chama ili kukipa taswira mpya chama na kuweza kuendana na kasi ya ushindani na mabadiliko ya sasa,nakurudisha matumaini ya chama kushika dola kwa siku zijazo

Kwanza lazima tujue wamiliki wa chama ni sisi wananchama ambao ndio wapiga kura,viongozi watakuwepo kwa niaba yetu

Zipo sababu zinazo tusukuma tuamini hivyo na ndio njia pekee ya kukirudishia chama hadhi yake inayo endelea kupotea kwa kasi na chama kuweza kushika dola kwa siku zinazo kuja

Leo ntataja sababu 10 japo zipo nyingi zinazo uondolea uwezo uongozi uliopo wa ngazi ya juu ya chama kuwa na imani ya kuendelea kuongoza chama kwa ushindani

1 .Wameshindwa kuonesha ukweli wa madai ya kuwa kuwafukuza Dr .Kitila Mkumbo Zitto na Samsoni Mwigamba kunge kiimarisha chama zaidi huku ndani ya miezi 5 chama kimezidi kupotea zaidi tangu wafukuzwe

Uharali wa njia iliyo tumika kupata suluhu ya mgogoru huu tukiipima ma matokeo ya chama kwa sasa hakuna anaye weza kubisha kwamba chama kimezidi kupoteza zaidi kuliko yalivyo kuwa madai ya baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu
Na hivyo kuleta taswira ya kushindwa kwa maamzi sahihi na kugeuka kuwa hujuma kwa chama

Hakuna ushahidi wowote uwe wa kisayansi au kawaida unao onesha chama kuimalika kwa hatua hiyo iliyo chukuliwa dhidi ya viongozi hawa zaidi matokeo ya awali yanaweza kuwa yakionesha chama kupoteza zaidi,Na mifano ni katika chaguzi na mapokeo ya watu katika mikutano ya katibu mkuu huko mikoani

Hakuna mwenye uwezo wa kubisha kama chama kwa sasa kina mpasuko mkubwa na hivyo kuelekea kupotea kabisa .

Ni jukumu lenu wana chama na wenye chama kulitizama hili kwa njia zote mbili kwa maana ya faida na hasara

2 . Hawaoneshi kama wana kerwa tena na kushindwa kwa chama katika chaguzi ndogo ambazo zimekuwa zikifanyika hapa nchini

Leo viongozi wa juu hakuna yajali tena chama kushindwa.imekuwa ni kwaida kusindikiza na baada ya matokeo wako kimya kama vile matokeo waliyajua kabla.Mifano ni mingi wamekuwa wakishiriki kama kusindikaiza na wakati mwingine hawashiriki kabisa pengine kama hawana ahabari kabisa

3. Sababu zinazo tolewa na viongozi mara baada ya kushindwa sio harisia nyingi zimejaa lawama na visingizio kibao na ni wakati mwingine ni dhaifu mno kiasi zinakatisha tama wanachama kuendelea kushiriki
Na sababu zenyewe ni kama :

(1) Tunashindwa kwa sababu daftari la kudumu la wapiga kura halija boreshwa

Hatupingi haki ya watu walio fikisha umri wa kupiga kura na wasipige hapana! Wapo wanao liona swala hili limekaa ki propaganda zaidi na sio ki technical, na hoja ni kwamba wakati tunaingia kwenye kampeini tunakuwa na malengo sawa kwa vyama vyote vinavyo shiriki iweje swala hili litukwaze sisi tu na liwe faida kwa upande mwingine? Ikiwa lengo ni kwenda ku wine wapiga kura ambao wawe wengi au wachache hao hao iweje kwetu waonekane wakiwa wachache na wengi kwao?Na je tunao ushihidi wa moja kwa moja kama wote walioko nje ni wetu?

(2) Tuna shindwa kwa sababu uelewa wa wananchi ni mdogo

Kwanza haya yamekuwa yamekuwa yakitafsriwa kama matusi kwa wapiga wenu wenu

Lakini mbona tumekuwa tukipewa mda wa kutosha wa kamepeni,mda ambao unatosha kabisa kuzunguka nyumba hadi nyumba tukitoa hiyo elimu?Na mbona baada ya uchaguzi tuko mjini? Na mbona tuhuma hizi zinakuja tu pale kwenye maeneo tunayo shindwa tu? Na mbona elimu ya wenzetu inaeleweka?

- Tatizo linaweza kuwa ni la walimu wetu tunao watuma huko huenda hawaeleweki au hawana mvuto au wanatumia lugha isokuwa na staha kuomba kura au tumewachagua kwa hira
(3) Washindani wetu ambao ni CCM wanatumia vyombo vya dola na wana saidiwa na serikali na tuna kwenda mbali kidogo wapiga kura wetu wana tishwa

Lakini kwa mara nyingi tuhuma hizi huwa zinakuja pale tunapo kuwa tume shindwa natukishinda wanakuwa ni walinzi wa usalama

Polisi huenda ikawa ni kweli wanazuia mikutano yetu lakini sio mara zote hata tunapo kuwa katika mikutano ya harali na kwa mda ulio pangwa

4 Chama kimeshindwa kujisimamia tena katika ajenda zake na badala yeake sasa kimekuwa chama cha matukio na hivyo kutishai uhai wa chama pindi matukio yatakapo kuwa hayapo tena

Naomba mambo mengine 6 yaliyo baki niyataje tu nisiyatolee maelezo kuchelea kuwa na maelezo mengi zaidi

5 Progaram zilizo buniwa za kukiendesha chama nchi nzima hazioneshi kama zimefanikiwa na kupewa kipa umbele na hivyo chama kubakia cha ukanda tu

6 Swala la uchaguzi wa ndani ya chama ambao ungetoa taswira mpya ya chama kwa siku zinazo kuja mbeleni ni kama mchezo wa kuigiza . Na hivyo hatuoni juhudi. za kufanya hivyo pamoja na kuwa vyama vingine vishafanya hivyo na wateule tiyari wako wanavitumikia vyama vyao

7 . Zipo dalili ambazo kwa zinaoensha kwa makusudi kama viongozi wanaweza kubakia wale wale pamoja na changamoto tulizo zitaja hizo kuwalemea

8 Chama chini ya viongozi wetu hawa kwa sasa kinatembelea magongo katika chaguzi zote ,Chama kimeonesha kuwa kinatembea mwendo wa kinyonga kwenye bio za farasi

9 Chama chini ya viongozi wetu hawa kinaonekana kukosa mbinu mpya za kuvuna wanachama wapya toka vyama vingine na hivyo kuonesha kama chama kunadumaa na waliomo wanaondoka

10 Matumizi ya fedha yanayo tumika kwenye chaguzi ndogo ni makubwa na ukiringanisha na matokeo ya kura yanayo patikana na hivyo kushawishi kuona hapa panahitaji mabadiriko makubwa ya fikra na uongozi(chopa 3 kata 3)

Baada ya kuyasema hayo ni Rai yangu kuona jukumu la kukiokoa Chama linabaki mikononi mwa wanachama na viongozi makini kujipima kulingana na changamoto zilizoko kwenye chama kwa sasa

Niwakumbushe tena nikihitimisha nimeileza kwa kirefu dhamira yangu hii iliyo beba dhamira ya kukumbusha ili kutoa mwanya kwa wale wanao taka kunikosoa wanikosoe ,kupinga na wapinge,kuunga mkono na waunge

Lakini zipo dalili za wazi kabisa kama viongozi wetu wa juu wame pwaya katika kukiendesha chama na hivyo ni Rai yangu tuwapongeze kwa kazi nzuri walio ifanya huko nyuma walipo kitoa chama na walipo kifikisha na wakubari kwa hiari yao Au wana chama wenye chama waamue kusema inatosha kama ambavyo nimeona mimi inatosha kwao

NB: Maoni haya asihusishwe mtu mwingine yeyote zaidi yangu,ni yangu na nimeyaleta kwenu wapenda mageuzi ya kweli nchini na wale wale wanao penda kuyaona mabadiliko ya kweli na Chadema ikishika dola kwa siku zinazo kuja

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments