- Kwa nini mnapinga muundo wa Muungano wakati walioupendekeza ni wananchi?
- Kwa nini Tanganyika imevaa koti la Muungano?
- Je hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi?
- Je tume ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?
- Kwa nini kuituhumu Tume ya Warioba pekee kuwa imependekeza muundo wa serikali tatu wakati Tume za Jaji Kisanga na Jaji Nyalali nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu?
- Kwa nini hamtaki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badala yake mnageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba?
- Kwa nini mnaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
Haya kazi kwenu siye wananchi twasubiri majubu hay kwa hamu sana ili tuwe na amani na imani kuwa mtatutengenezea katika ya wananchi.
0 Comments