[wanabidii] MKUTANO MKUBWA WA UKAWA UNGUJA NA PEMBA

Tuesday, April 29, 2014

Haya haya wazanzibari! Kumekucha! La mgambo likilia kuna jambo! Chama cha wananchi CUF kikishirikiana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kinawatangazia wanachama, wapenzi na wazanzibari wote wa mikoa mitatu ya Unguja na mikoa miwili ya Pemba, wazalendo na wapenda nchi yao kwa jumla kuhudhuria kwa wingi katika mikutano miwili mikubwa ya hadhara ya aina yake na ya kihistoria itakaofanyika kesho siku ya Jumatano ya tarehe 30/04/2014 katika viwanja vya Kibanda Maiti, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Maghribi Unguja na kesho kutwa Alhamisi tarehe 31/04/2014 katika viwanja vya Tibirinzi Pemba.

Wageni rasmi katika Mikutano hio ni Mwenyekiti wa CUF na kiongozi wa UKAWA, Prof Ibrahim Haruna Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Mh James Mbatia na Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila.

Simba wa nyika, tishio la vibaraka wauza nchi yetu, kipenzi cha wazanzibari, mwenye uzalendo wa hali ya juu na mapenzi makubwa kwa Zanzibar na wazanzibari, Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad nae atanguruma.

Wapambanaji wengine wanaounda UKAWA, wakiwemo Mh Ismail Jussa, Mh Julius Mtatiro na Mh Tundu Lissu nao watanguruma mikutanoni. 
Mikutano utaanza saa 8 barabara za mchana mpaka saa 12:00 jioni.

Agenda kuu katika Mikutano hio Maalum ni je Bunge la Katiba lililogeuzwa na CCM kuwa Bunge la Intarahamwe litafanikiwa kupindisha matakwa ya watanzania ya serikali tatu walioyatoa kwa Tume ya Jaji Warioba? Je watanzania watarajie nini baada ya Mashujaa wapigania Katiba ya wanacnhi kulisusia Bunge La Katiba?

Maswali yote hayo yatapatiwa majibu pamoja na mambo kadhaa muhimu. Hatumwi mototo!

Shime wazanzibari wote kuhudhuria kwa wingi bila ya kukosa!
Live at www.chuchufm.com. Matayarisho ya live TV yanaendelea tutajulishwa.

SERIKALI TATU HAZIEPUKIKI!

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments