[wanabidii] Je, Watanzania wanaionaje katiba?

Thursday, April 24, 2014

Twaweza: What do people really think of the constitution? Je, Watanzania wanaionaje katiba?

Mjadala katika Bunge la Katiba umejaa na ubishi na mgawanyiko, lakini Watanzania wameungana kutaka katiba yenye uwajibikaji zaidi kwa viongozi wa umma na mfumo wa utawala wenye uwazi zaidi. Miongoni mwa vifungu katika rasimu pili ya katiba ambavyo vinaungwa mkono na wananchi walau sita kati ya kumi ni:
  • Idadi kubwa ya Watanzania wanaunga mkono vifungu vinavyohusiana na haki ya wananchi kupata taarifa au habari, na kuongezeka kwa uwajibikaji na uwazi wa viongozi wa umma
  • Mapendekezo kwa ajili ya utaratibu wa kudhibiti na kuwajibisha wabunge na mgawanyo wa madaraka ili kuepuka migogoro ya kimaslahi yanaungwa mkono na wengi
Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Je, Watanzania wanafikiri nini hasa juu ya katiba? Matokeo ya utafiti wenye uwakilishi wa kitaifa

Muhtasari umetokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti kwa njia ya simu ya mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa uliofanyika kote Tanzania Bara, naWasemavyo Wazanzibari, Utafiti kwa njia ya simu ya mkononi wenye uwakilishi wa kitaifa uliofanyika visiwani Zanzibar, ukiendeshwa na Taasisi ya Kimataifa ya Sera na Sheria (The International Law and Policy Institute).

Sauti za Wananchi imebaini kuwa, uungwaji mkono ni mkubwa sana miongoni mwa wananchi wa Tanzania Bara kwenye vifungu vingi vilivyowasilishwa katika rasimu ya kwanza ya katiba na vimebaki katika rasimu ya pili. Vifungu hivyo ni vile vinavyohusu kuwepo kwa uwajibikaji zaidi kwa watumishi wa umma, kuimarisha utaratibu wa dola ili kudhibiti na kuwajibisha wabunge, hasa wabunge kuwajibika kwa wapiga kura wao, na kuongeza ushindani zaidi wa kisiasa.

Utafiti pia unaonesha kuwa Watanzania wangeipitisha rasimu ya katiba bila shida ikiwa Watanzania sita kati ya kumi wameonesha kuwa wangeipigia kura ya Ndiyo. Tanzania Bara ni wananchi asilimia 65 na Zanzibar ni wananchi asilimia 62 wanaoikubali rasimu ya sasa.

Pakua nyaraka
Download documents

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments