[Mabadiliko] Je, Tutasindikiza Sherehe za MUUNGANO JUMATATU tena?? kama Ilivyokuwa siku ya Mapinduzi??

Saturday, April 26, 2014
JK atatangaza Tena Watanzania Kupumzika siku ya Kazi Kusindikiza Muungano wa Zanzibar na Tanganyika? Atashauriana na akina Nani?

Nakumbuka siku ya Jumatatu Tar 13, January, 2014 ilitangazwa kuwa ni siku ya kupumzika ili kusindikiza sherehe za Mapinduzi Zanzibar baada ya siku hiyo ya Tar 12 January 2014 kuangukia Jumapili. Rais wa JMT na Rais wa SMZ walisema kuwa wameshauriana kuwa Jumatatu watu wasiende kazini ili wafurahie miaka 50 ya mapinduzi ya Zanzibar; hiyo ilikuwa ni ya Zanzibar tu, Nchi ambayo ni sehemu ya Tanzania.

Leo ni siku ya Jumamosi, Tar 24 April 2014, siku ambayo tunakumbuka Muungano ya Tanganyika (ya kusadikika) na Zanzibar zilipoungana na kuunda TANZANIA. Kwakuwa siku hii imeangukia Jumamosi, siku ambayo si ya kazi, Je, tunadhani JK atatangaza Jumatatu kuwa siku ya mapumziko? na si Jumatatu tu, kwakuwa Shein Alishauriana na JK tu na kuamrisha kuwa jumatatu ni mapumziko, JK sasa ikitokea anataka kushauriana na viongozi wa nchi zilizounda Muungano wa Tanzania, atashauriana na SHEIN kama Rais anayewakilisha Zanzibar, vipi kwa upande wa Tanganyika, atashauriana na nani?

Katika hili nadhani linawezaonesha kama JK aliona kuwa walikosea kusema Jumatatu watu wapumzike, taifa masikini kama hili ambalo watu wake wengi ukiwaambia wakae nyumbani tu siku nzima, utawashindisha na njaa, endapo tu hatatangaza tena siku ya mapumziko. Lakini kwa upande mwingine, itaibua maswali kuwa, Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kubwa Kuliko ya Muungano? endapo tu hatasema watu wapumzike jumatatu.
Kwa mtazamo wangu, sioni haja ya kupumzika tena, itakuwa ni ujinga sana kwa nchi masikini ambayo inatakiwa ijikomboe kwa kufanya kazi, ikawa inatoa mapumziko yasiyo ya lazima.

JK akisema atashauriana na viongozi wa nchi zilizounga muungano, umewahi fikiria nani atashauriana nao hususani kutoka Tanganyika, iliyobatizwa jina la Tanzania bara?

Nawatakieni Sherehe Njema za Kukumbuka Siku ya Muungano. "MUUNGANO WETU, NDIO UMOJA WETU"

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Zanzibar,
Mungu Ibariku Tanganyika *****

Ameni!

--
Ipyana Lwinga
Email:    ipyanalwinga@gmail.com

"Mpende Jirani yako kama nafsi yako..."

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CAPd8eK-jjQPUR36v7j7n4U0ShMyHj1MsHKNQXqqtVuMuUqCRfA%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments