[wanabidii] WARAKA WANGU KWA RASTA CHACHA ZAKAYO WANGWE

Saturday, March 15, 2014
WARAKA WANGU KWA RASTA CHACHA ZAKAYO WANGWE

Ilikuwa ni siku ya simanzi kubwa iliyojawa na utata pale kilipotangazwa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Chacha Zakayo Wangwe (Rasta). Rasta umekwenda haupo tena, ulituacha na majonzi makubwa sana, kamwe sitosahau siku tuliyokuweka kwenye nyumba yako ya milele pale kijijini Nyarelo. Tulijitokeza umati mkubwa sana kukusindikiza ndungu yetu. 

Katika kuazimisha miaka 5 tangu kifo chako nimeona ni vyema nikuandikie waraka huu kama sehemu ya kuenzi jitihada zako. Sioni umakini wa chama chako kuhakikisha wanathamini mchango wako kwa kuienzi siku ya leo. Yawezekana kweli haukuwa mwenzao kama ulivyo kuwa unadai kamanda. Bla shaka siku ikitokea mwenyezi mungu amewatwaa wenzio wa ule ukanda wa gaza tutasikia kuna siku itatangazwa maalumu ya kuwa kumbuka. Wamesahau kabisa kuwa wewe ndiye ulikuwa chachu na nguzo muhimu ya ujenzi wa chama chako kule KANDA YA ZIWA kwa wakati huo. Waache wao wakusahau ila siye ndugu zako tutakukumbuka daima tafadhali popote pale ulipo pokea salamu zangu Rasta:

(a) Tuna kukumbuka kwa mengi lakini kubwa liliwemo kuipigania kikamilifu wilaya yetu ya Tarime ndani na nje ya bunge. Pia mchango wako mkubwa wa kuhakikisha demokrasia na uwazi unatawala ndani ya chama chako kamwe hauto sahaulika. Tarime iliyo iacha bado ina shida nyingi pamoja na madini yetu bado ni moja ya wilaya fukara. Kadri siku zinavyo zidi kwenda rutuba zinazidi kupungua pamoja na mvua haba, huenda kilimo siku za usoni kitashindwa tena kutusaidia kama njia ya kujiparia kipato. 

(b) Tuna kukumbuka vyema ulivyo pambana kuhakikisha chama chako kinaendeshwa kwa katiba na kuachana ule utawala wa kidikteta na kauli za NDIYO MZEE na Mhe Mwenyekiti amesema. Ulisimama kikamilifu kupinga matumizi mabaya pamoja na ufisadi unaokitafuna chama chako kwenye matumizi hewa ya ruzuku na kwa kigezo kuwa eti wanajilipa madeni ya Kampeni. Kwenye hili ulionekana hufai huenda tu ni kwa sababu yawezekana hukuwa mwenzao?? Sasa hivi yupo mwenzio SHIBUDA kila kukicha wana mwandama. Vita hii uliyo ianzisha imesabababisha wengine kuitwa waasi ndani ya chama na kupelekea kufukuzwa kwa baadhi ya wanachama vijana. Naambiwa hapa kuwa ruzuku ya chama chako imepanda lakini bado office yenu ni ile ile ya kupanga kamanda.

(c) Nakumbuka jinsi ulivyo pambana kikamilifu kuhakikisha ukabila na upendeleo wa dhati unaondolewa kabisa ndani ya chama chako. Lakini bado mpaka leo hilo lina lalamikiwa kukithiri ndani ya CHADEMA. Dada yako Ghati Masore alishafukuzwa kwa kusema ukweli juu ya hili. Na cha kustajabisha wengi ambao wameteuliwa kupitia vitu maalumu bado wanalalamikiwa kuwa na vinasaba vya damu na kimapenzi na baadhi ya vigogo ndani ya chama chako. Nakumbuka uliacha tu kuna wakwe na watoto wa vigogo ndani ya chama chako siku hizi kuna mashangazi, wajomba, mabinamu, mashemeji hata wakina darling ndani ya chama chako. 

Nina mengi ya kukuandikia MURA WEITU lakini wacha kwa leo nisikuchoshe tutakukumbuka daima CHACHA ZAKHAYO WANGWE.
WARAKA WANGU KWA RASTA CHACHA ZAKAYO WANGWE    Ilikuwa ni siku ya simanzi kubwa iliyojawa na utata pale kilipotangazwa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Chacha Zakayo Wangwe (Rasta).  Rasta umekwenda haupo tena, ulituacha na majonzi makubwa sana, kamwe sitosahau siku tuliyokuweka kwenye nyumba yako ya milele pale kijijini Nyarelo. Tulijitokeza umati mkubwa sana kukusindikiza ndungu yetu.     Katika kuazimisha miaka 5 tangu kifo chako nimeona ni vyema nikuandikie waraka huu kama sehemu ya kuenzi jitihada zako. Sioni umakini wa chama chako kuhakikisha wanathamini mchango wako kwa kuienzi siku ya leo. Yawezekana kweli haukuwa mwenzao kama ulivyo kuwa unadai kamanda. Bla shaka siku ikitokea mwenyezi mungu amewatwaa wenzio wa ule ukanda wa gaza tutasikia kuna siku itatangazwa maalumu ya kuwa kumbuka. Wamesahau kabisa kuwa wewe ndiye ulikuwa chachu na nguzo muhimu ya ujenzi wa chama chako kule KANDA YA ZIWA kwa wakati huo. Waache wao wakusahau ila siye ndugu zako tutakukumbuka daima tafadhali popote pale ulipo pokea salamu zangu Rasta:    (a)	Tuna kukumbuka kwa mengi lakini kubwa liliwemo kuipigania kikamilifu wilaya yetu ya Tarime ndani na nje ya bunge. Pia mchango wako mkubwa wa kuhakikisha demokrasia na uwazi unatawala ndani ya chama chako kamwe hauto sahaulika. Tarime iliyo iacha bado ina shida nyingi pamoja na madini yetu bado ni moja ya wilaya fukara.  Kadri siku zinavyo zidi kwenda rutuba zinazidi kupungua pamoja na mvua haba, huenda kilimo siku za usoni kitashindwa tena kutusaidia kama njia ya kujiparia kipato.     (b)	Tuna kukumbuka vyema ulivyo pambana kuhakikisha chama chako kinaendeshwa kwa katiba na kuachana ule utawala wa kidikteta na kauli za NDIYO MZEE na Mhe Mwenyekiti amesema. Ulisimama kikamilifu kupinga matumizi mabaya pamoja na ufisadi unaokitafuna chama chako kwenye matumizi hewa ya ruzuku na kwa kigezo kuwa eti wanajilipa madeni ya Kampeni.  Kwenye hili ulionekana hufai huenda tu ni kwa sababu yawezekana hukuwa mwenzao?? Sasa hivi yupo mwenzio SHIBUDA kila kukicha wana mwandama. Vita hii uliyo ianzisha imesabababisha wengine kuitwa waasi ndani ya chama na kupelekea kufukuzwa kwa baadhi ya wanachama vijana. Naambiwa hapa kuwa  ruzuku ya chama chako imepanda lakini bado office yenu ni ile ile ya kupanga kamanda.        (c)	Nakumbuka jinsi ulivyo pambana kikamilifu kuhakikisha ukabila na upendeleo wa dhati unaondolewa kabisa ndani ya chama chako. Lakini bado mpaka leo hilo lina lalamikiwa kukithiri ndani ya CHADEMA. Dada yako Ghati Masore alishafukuzwa kwa kusema ukweli juu ya hili.  Na cha kustajabisha wengi ambao wameteuliwa kupitia vitu maalumu bado wanalalamikiwa kuwa na vinasaba vya damu na kimapenzi na baadhi ya vigogo ndani ya chama chako. Nakumbuka uliacha tu kuna wakwe na watoto wa vigogo ndani ya chama chako siku hizi kuna mashangazi, wajomba, mabinamu, mashemeji hata wakina darling ndani ya chama chako.       Nina mengi ya kukuandikia MURA WEITU lakini wacha kwa leo nisikuchoshe tutakukumbuka daima CHACHA ZAKHAYO WANGWE.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments