Wapentekote wapingana uteuzi wa rais Kikwete
Na Tanpress
KANISA la Pentecost Evangelist (PEC) limesema kwamba Mwenyekiti wa chama cha Democratic Party (DP) Mchungaji, Christopher Mtikila,ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwakilisha mawazo ya wapentokoste,katika bunge la katiba.
Akizungmza na wanahabari leo Dar es Salaam, Askofu wa jimbo la nyanda za juu, Mbeya,William Mwamalaanga amesema kuwa anasikitishwa na wale wanaolalamikia uteuzi wa Rais Kikwete kwamba amewatenga wapentekoste wakati alimteua Mchungaji Mtikila.
"nawashangaa Wapentekoste wenzangu wanaodai kumlaani Rais kwamba hajawateua wawakilishi kutoka kwenye kanisa letu , wakati kamteua Mtikila ambaye anauwelewa mzuri kuliko wajumbe wengi kuhusu mambo ya katiba na serikali ya Tanganyika"amenukuliwa
Askofu Mwamlanga ambaye amejitambalisha kuwa ni Mwenyekiti wa kamati ya wanataaluma,haki za binadamu na mazingira inayoundwa na viogozi wa dini amesema kwamba Mtikila alianza kutetea serikali ya Tanganyika tangu Mwaka 1986.
"Nimesikia kwamba baadhi ya wapentekoste wamemlaani Rais Kikwete kwa kuwatenga katika bunge la Katiba,….sio kazi yetu viongozi wa dini kulaani serikali ….kazi yetu ni kuombea na kutoa Baraka…mtu anayelaani serikali yake ni sawa na yule anayelaani sahani anayotumia kulia chakula"amesema Mwamlanga.
Aidha amewatahadharisha viongozi wa dini kujitenga na siasa kwani kama nchi ikichafuka kutokana na kauli zao hawatapata pa kukimbilia kwani hata wao wataakuwa sehemu ya watanzania.
Askofu Mwamlaanga ametoa tamko hilo saa chache baada ya Askofu mwenzake Zakary Kakombe kusambaza waraka wa kuilaani serikali kwa kitendo chake cha kuwatenga wapentekoste katika bunge la katiba huku baraza la maaskofu wa kipentekoste wakitajwa kumuunga mkono waraka huo.
0 Comments