[wanabidii] VIPINDI VYA KWENYE TV VYA "LADY JAY D" & "WEMA" NANI ANAYENUFAIKA NAVYO?

Monday, March 03, 2014
Hivi ni vipindi vya wasanii wenzetu, lakini kusema ukweli, mathalani kwangu, sioni mantiki yake kwa jamii yetu ya Kitanzania? Tunaweza tukawa tumeiga utamaduni na staili hii kutoka kwa wenzetu, lakini najiuza, hivi hawa wasanii walioneemeka kwa fedha za walala hoi Watanzania, wamekosa namna nyingine ya kujipatia umaarufu na kurudisha fadhila kwa Watanzania zaidi ya jinsi hii ya kujianika kwa gharama za kupindukia kwenye runinga?

Fedha wanazotumia kujianika kwa gharama kwenye runinga huku wadogo zao shule za kata wakikalia mawe, na miaka michache, mabinti zetu wanaokalia mawe, watakuwa wazazi, na bila shaka wataandamwa na gonjwa la fistula, ni busara hii kwa wasanii wetu? Yapo mambo mengi ambayo wangeliweza kufanya zaidi ya kutuonyesha mambo yao binafsi kwenye runinga! Ndio, kuna msemo kuwa, msanii ni kioo cha jamii, lakini nina mashaka kama wanayotuonyesha yanaakisi jamii ya Kitanzania. Tena wanachokiwasilisha, sio cha Kitanzania!

Naomba kuuliza, ni kwa manufaa ya nani? Na kwa nini fedha zinazotumika kurusha matangazo, samahani kwa neno hili, yasiyo na tija kwenye runinga, zisielekezwe kwingine ambako zingeliwapatia sio tu umaarufu kwenye dunia ya leo bali na ule ulimwengu ujao? Kumbuka, kuweka hazina yako isikoweza kuliwa na kutu au nondo!

Naomba tujadili hili.

-----------------------
Fratern Kilasara
,

P. O. Box - (Home): 62810; or (Office): 65300
Dar es Salaam - Tanzania.
Telephone (Office): +255 (0)22 2700021/4 Ext No. 239; Fax: +255 (0)22 2775591
Mobile (Personal): +255 (0)715 40 41 53 or +255 (0)754 40 41 53
Emails: kilasara.fratern@gmail.com or kilasara.fratern@yahoo.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments