Ndugu zangu ,
Leo tuzungumzie Ujasusi/Upelelezi , Jinsi tunavyoweza kutumia wasanii wetu wa fani mbalimbali kwenye shuguli za kijasusi au upelelezi zenye maslahi kwa Nchi zetu .
Mwaka 2010 mpaka 2013 kulikuwa na wimbi la wasanii wengi sana kuingia nchini kwa ajili ya shuguli mbalimbali ambazo inasemekana ni za kimuziki , wengine kutembelea mbuga za wanyama , wengine kutembelea miradi mbalimbali ya kimaendeleo na hata wengine kutoa fedha na misaada kadhaa kwa wahitaji .
Nchi kama marekani inawasanii ambao ni mabalozi wa mashirika kadhaa ya umoja wa mataifa ambapo wanapata fursa ya kusafiri sehemu mbalimbali duniani haswa zenye maslahi kwa nchi hiyo kwa ajili ya shuguli hizi za upepelezi / ujasusi lakini kwa kivuli cha kutoa huduma .
Msanii kama ben aflek yeye ana shirika lake la maziwa makuu linashugulika zaidi nchini kongo kwenye migodi ya alamasi na dhahabu , msanii kama bono wa kundi la U2 anajulikana kwa harakati zake za njaa na chakula duniani huku akiwa na hisa kwenye kampuni za vyakula na kilimo .
Hapa nchini Msanii Fresh Prince au will smith aliwahi kuja na kutoa fedha kwa Taasisi ya Ifakara inayofanya utafiti wa malaria , zile fedha inaweza kuwa ni uwekezaji wa utafiti wa kitu Fulani ambao kama ukifanikiwa inaweza kuwa biashara ya kulipa siku za mbele na sehemu ya kipato kwa familia ya will smith na uchumi wa marekani ( Haya ni Mawazo yangu ).
Sasa turudi hapa kwetu kwa mara nyingine , Tunatumiaje wasanii wetu wanaovuka mipaka katika kazi zao kwenye shuguli za ujasusi/Upelelezi kwa ajili ya biashara au taarifa nyingine kwa maslahi ya nchi kama wanavyofanya wasanii wan chi za wenzetu ?
Swahili hili nakuachia wewe , Najua kuna watu wataanza kubisha oohh haiwezekani , tunapewa misaada tu , tunapendwa ETC .
Institut d'études de sécurité - SA
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments