[wanabidii] Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Dodoma ajirusha kutoka ghorofani

Thursday, March 20, 2014
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu Dodoma – UDOM aliyefahamika kwa jina la KAMUGISHA S/O ISACK, Miaka 24, Mhaya, Mwaka wa Tatu, Kitivo cha Sayansi ya Jamii (Social Science) anayeishi Block Namba 11, chumba Namba 62, alijitupa kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kusababisha majeraha sehemu 
za mdomoni, shingoni na paji la uso.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amesema tukio hili limetokea terehe 18/03/2014 majira ya 20:15 huko maeneo ya chuo kikuu cha Dodoma manispaa na Mkoa wa Dodoma.

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni ulevi. Majeruhi alilazwa katika hospitali ya UDOM na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na kuruhusiwa tarehe 20/03/2014 baada ya kuonekana hali yake inaendelea kuimarika.

Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya kukamilisha taratibu zote kujibu shitaka la kujaribu kujiua.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments