[wanabidii] Afa akiongea kupitia simu iliyopata hitilafu wakati ikichajiwa

Tuesday, March 18, 2014
Ali Bakari Ali (20) mkazi wa Kisima Majongoo mjini Unguja amekufa baada ya simu yake aliyokuwa akitumia ambayo ilikuwa imeunganishwa na chaja ya umeme kupata hitilafu.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam amethibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema Ali alikufa baada ya kupata mshtuko wa umeme unaotokana na simu yake iliyokuwa imewekwa katika 
chaja ya umeme huku akifanya mawasiliano. 

"Ni kweli tumepata taarifa ya kifo cha kijana Bakari Ali ambaye alikuwa akisikiliza simu yake iliyokuwa imewekwa katika chaja ya umeme na kusababisha mshituko mkubwa," alisema. 

Kamanda Mkadam alitoa wito kwa wananchi kuepusha ajali kama hizo kwa kuwataka kuwa waangalifu na pia kuziondoa simu zao kwenye umeme wakati wanapozisikiliza.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments