[wanabidii] KURUDISHWA KWA USAFIRI WA MABASI KWENDA FERRY NA MNAZI MMOJA

Thursday, February 13, 2014

YAH: KURUDISHWA KWA USAFIRI WA MABASI KWENDA FERRY NA MNAZI MMOJA


Kutokana na adha wanayopata abiria wanaofanya safari zao kati ya Kivukoni na Mnazi Mmoja, SUMATRA ikishirikiana na kikosi cha usalama barabarani (Kanda maalumu) imerudisha usafiri huo ambapo mabasi ya UDA sita (kwa kuanzia) yatakuwa yanafanya safari kila siku katika maeneo hayo.

Usafiri huu umeanza rasmi leo tarehe 12.02.2014 asubuhi, japo kulikuwa na matatizo ya hapa na pale lakini
kwa kuwa wote (SUMATRA, Polisi na UDA tulikuwa barabarani tuliweza kurekebisha kasoro hizo kwa pamoja.

Njia zitakazotumika ni kama ifuatavyo:

Kutoka Mnazi Mmoja: Zittanzia Mnazi Mmoja kisha zitakwenda hadi kituo cha Baridi na kuendelea na safari kwa kutumia barabara ya Bibi Titi hadi Maktaba kisha zitaingia kulia kwenda Posta Mpya na kwenda Ferry.

Kutoka Kivukoni (Ferry): Yatatumia njia hizo bali zitakapofika makutano ya barabara za Bibi Titi na Uhuru (Traffic light) zitaingia kulia hadi makutano ya barabara za Uhuru na Lumumba kisha zitaingia kushoto hadi eneo zilipoanzia safari kwa ajili ya kuchukua abiri akwenda Ferry.

Tunatarajia idadi ya mabasi itakuwa inaongezeka kuendana na mahitaji, na nakuli itakayotumia ni shilingi 400/= tu.

Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki

K. Shio
Kny: MKURUGENZI MKUU

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments