[wanabidii] U WAPI UHALALI WA CHADEMA KUZUIA KUSHITAKIWA MAHAKAMANI

Monday, January 06, 2014
UU WAPI UHALALI WA CHADEMA KUZUIA KUSHITAKIWA MAHAKAMANI..!!

UTANGULIZI,
Mimi ni mwanachama wa chadema ninaeamini katika mfumo unaopigania mabadiliko yaanzie ndani kisha yatoke nje, hii ni makala itakayotoka kwenye gazeti week hii, leo nitaiweka kwa kifupi tu lakini itapatikana baadae kwa uzima wake.

UKAMILI,

Nimekuwa nikisimama na kukitetea chama kwa mambo ya msingi yanayotakiwa kutetewa, lakini sijawahi kukitetea chama wala kukigandamiza kwa mambo yanayofanywa na viongozi yaliyo ya kipuuzi,badala yake kwenye jambo lenye mikanganyiko huwa nakaa kimya huku nikingojea na kushiriki namna ambavyo tutayabadilisha.

Naamini kuwa huwezi kukimbia matatizo kwa lengo la kuyakabili na kuyaondoa, badala yake unatakiwa ukabiliane nayo ukiwa kwenye mfumo na ndio sababu ya mimi kuwa mwanachama mvumilivu ninaepambana nikiamini mabadiliko yataletwa na sisi wenyewe,

Sikuwahi kuhoji hadharani hili la katiba ya chama kuzuia mwanachama kukishitaki chama mahakamani, lakini niliwahi kuwauliza watu wengi wenye upeo wa sheria na wanasheria wenyewe,

Sijawahi kuunga mkono mambo mengi likiweo hili na sijawahi kulitamka hadharani kama hivi nifanyavyo leo, kwa sababu niliamini katika kufuata taratibu za chama kumaliza utata unaojitokeza katika katiba na kanuni za chama chetu,

Lakini mfumo unapoonekana kupuuzwa kwa sababu tu ya hoja inayotolewa inaweza kufunga mirija ya wakubwa kunyonya mafuta ya kondoo aliyenona, basi mifumo hiyo haina maana tena itabidi itafutwe njia nyingine nje ya mfumo na taratibu za taasisi,

Kuhusu suala la achama kuzuia kushitakiwa na mwanachama mahakamani, nililipinga siku nyingi kupitia mifumo halisi, hata mwaka jana niliandika vipengele vyenye utata kwenye katiba ya chama nilituma kwa katibu mkuu...yenye kichwa cha habari ''UU WAPI UHALALI WETU?'' nilieleza namna ambavyo chama kinadai mambo kadha wa kadha huku viongozi wakisahau yanamikanganyo kwenye katiba yetu, nikagusia kitendo cha Mbunge wa Nyamagana kutoa tamko la kuwataka wamachinga wafanye biashara misikitini na makanisani, huku akiwa hajui (nadhani sio kosa lake maana ni mgeni kwenye chama na hasomi katiba anafanana na Sugu, Lema na Msigwa) katiba ya chama inasema "tunaamini katika soko huria na sio soko holela''.

Turudi kwenye maada yetu sasa, ukiuliza kwa nini sikuwahi kusema na kwa nini niseme leo, jibu ni kama ifuatavyo...niliamini kuwa ipo siku tutayabadilisha, lakini kwa kuwa mfumo unapoonekana kupuuza mawazo na maono ya wasio wa milengo yao basi mifumo hiyo haina maana tena, sasa nasema hata mie nimeona mfumo wetu hauna maana tena na hatuwezi kuubadili kwa njia waitayo taratibu za chama..sasa nahoji..!!

Tunapata wapi uhalali wa kuzuia mwanachama asishitaki chama mahakamani? je tunaamini kuwa tutaongozwa na malaika asiyekosea? tutakuwa na viongozi wasioweza kuwa madikteta wanyonga watu? je wanasheria waliopitisha hii kanuni na katiba inayosomeka hivi walikuwa na nia ipi?

Tunatengeneza kanuni na vijisheria vinavyotupa uhalaili wa kutoshitakiwa mahakamani huku sisi tukidai Rais ashitakiwe...(huu ni ujuha wa hali ya juu)

Maamuzi ya viongozi wa chama yasihojiwe mahakamani huku sisi tukipigia chepuo katiba ya nchi itamke vyema kuwa matokeo ya uchaguzi mkuu yapingwe mahakamani (nao ni ujuha wa kimo cha juu sana) 

Chama chenye viongozi wasiamini katika kuwepo kwa vyombo vya sheria ni dalili ya ushetani na udikiteta usiofaa kuungwa mkono, natapa picha kuwa pengine tukipewa dola tutafuta mahakama kabisa na kufanya chama kuwa ndicho chombo cha mwisho cha maamuzi juu ya maisha ya watu,

Simlaumu Mzee Slaa wala Huyo Mwanasheria Tundu Lissu bali nalaumu fursa zao na historia zao walizopitia mpaka hapo.

Hii ni sehemu tu ya MAKALA ITAKAYOTOKEA KWENYE GAZETI

By Grayson M. Nyakarungu 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments