[wanabidii] Tuwekeze Zaidi katika Lugha za Asili

Monday, January 20, 2014
Naona ndugu huthamini moja ya jitihadi alizofanya hayati Mwl. Nyerere. Katika nchi za kiafrika, Tanzania inasifika kuwa watu wake wote wanaelewana wakitumia kiswahili. Jamii ya Ki-Tanzania haitofautiani na jamii nyingi za nchi za ulaya ambazo watu wake wote wanaelewana. Hii ni hatua nzuri sana. Katiba haimkatazi mtu yeyote kuongea lugha yake ya kiinyezi, lakini katiba inatumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza na sio za kiinyeji kwa sababu katiba ni kwa watu wote na tunapoongea au kujadili masuala mbalimbali ya uma ni lazima tuelewane. Kurejea nyuma ni kusimamisha maendeleo. Ingekuwa vizuri kuongeza kamusi (maneno) ya kiswahili kutoka kwenye lugha za kiinyeji pale inapowezekani. Kwa mfano, MSICHANA kwa KIMASAI wanasema NDITO , neno hilo linaweza kuidhinishwa na baraza la kiswahili na kuweza kutumiwa na watu wote. Nchi haina pesa kuanza kupromote lugha za kienyeji. Tutaanza kurudi kwenye ukabila tu.

Mtanganyika

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments