[wanabidii] Rais Kikwete kuteua wajumbe wa Bunge la Katiba wiki kesho kati ya waliopendekezwa

Thursday, January 23, 2014
Rais Jakaya Kikwete, wiki ijayo atakamilisha uteuzi wa majina ya wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba, uteuzi unaoashiria kuanza kwa bunge hilo litakalokuwa na wajumbe 640.

Bunge hilo litakaloanza mwanzoni mwa mwezi ujao mjini Dodoma, litakuwa na kazi ya kuijadili na kuipitisha Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Desemba 30 mwaka jana.

Wajumbe wengine watakaounda Bunge hilo ni 42 kutoka vyama vya siasa, 358 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na
 81 kutoka Baraza la Wawakilishi.

Januari 2 mwaka huu, ilikuwa siku ya mwisho kwa Ikulu kupokea majina ya makundi mbalimbali ya kijamii ambayo yaliwasilisha mapendekezo ya majina ya watu ambao wangependa wawe wajumbe wa Bunge hilo. Makundi zaidi ya 50 yaliwasilisha majina yao.
MCHANGANUO WA MAPENDEKEZO YALIYOWASILISHWA  YA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA 

(TANZANIA BARA)

NA.
AINA YA KIKUNDI/TAASISI
IDADI INAYOTAKIWA KISHERIA
IDADI YA MAPENDEKEZO YALIYOWASILISHWA
IDADI YA MAJINA YALIYOWASILISHWA
1.
Taasisi Zisizokuwa za Kiserikali
20
245
1185
2.
Taasisi za Kidini
20
77
277
3.
Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu
42
21
126
4.
Taasisi za Elimu
20
9
82
5.
Makundi ya Watu wenye Ulemavu
20
24
70
6.
Vyama vya Wafanyakazi
19
20
69
7.
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji
10
8
43
8.
Vyama Vinavyowakilisha Wavuvi
10
7
45
9.
Vyama vya Wakulima
20
22
115
10.
Makundi Yenye Malengo Yanayofanana
20
142
710


JUMLA
201
575
2722


Kuanza kwa Bunge hilo kunatarajiwa kuwa na mvutano mkali kutokana na msimamo wa baadhi ya makundi hayo, hasa vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikipingana zaidi katika mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, ilisema kuwa pia majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba nayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013. Sheria hiyo inampa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano kushauriana na Rais wa Zanzibar, kuteua wajumbe 201 wa Bunge la Katiba.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments