[wanabidii] Rais Kikwete aalikwa Nigeria na Rais Jonathan

Sunday, January 26, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Kikwete aalikwa Nigeria na Rais Jonathan

Rais wa Nigeria Mheshimiwa Goodluck Jonathan amemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Taasisi ya Uchumi Duniani Afrika (WEF-Africa) unaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria wa Abuja mwezi Mei mwaka huu.

Rais Jonathan ametoa mwaliko huo kwa Rais Kikwete wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo leo, Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako viongozi hao wanahudhuria wa 
Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF. 

Rais Kikwete amekubali mwaliko huo wa kuhudhuria Mkutano huo uliopangwa kufanyika Mei 7-9 mwaka huu mjini Abuja, Nigeria.

Mkutano huo kati ya viongozi hao wawili umehudhuriwa na Mawaziri wa Nigeria wa Mambo ya Nje na Fedha na Uchumi.

Nigeria inakuwa nchi ya nne katika Afrika kuandaa mkutano huo. Kwa miaka mingi, mkutano huo wa WEF-Africa ulikuwa unafanyika Cape Town, Afrika Kusini mpaka Tanzania ilipofanikiwa kuwa nchi ya kwanza ya Afrika nje ya Afrika Kusini kuandaa Mkutano huo mwaka 2010.

Tokea wakati huo, Ethiopia imeandaa mkutano huo na sasa Nigeria.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

23 January, 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments