[wanabidii] MAMBO YANAYOKINZANA KATIKA RASIMU YA KATIBA MPYA

Wednesday, January 22, 2014

MAMBO YANAYOKINZANA KATIKA RASIMU YA KATIBA MPYA

Neno kizuizini katika ibara ya 38.(1)(a) Mtuhumiwa aelezwe sababu za kukamatwa kabla ya kukamatwa hii itaondoa uwezekana wa mtu kubambikiwa kesi.na wakati anakamatwa lazima pawepo mashaidi anowaamini yeye watakaoelezea mazingira na sababu za kukamatwa kwake punde itakapobidi.

(e)apelekwe mahakamani ndani ya saa 12.na kama si siku za mahakama apewe dhamana na polisi wenyewe bila ya masharti isipokuwa kwa kesi za mauaji.

Ibara ya 57 iwe hvi

(a)    Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania

(b)   Serikali ya Visiwani

(c)    Serikali ya Bara

Maneno Tanzania bara na Zanzibar yaondolewe.Vinginevyo kama neno Zanzibar  litatumika na neno Tanganyika litumike pia.

66(3)Viongozi wakuu watakuwa

(a)Rais wa Jamhuri ya Muungano

(b) Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano

© Kiongozi wa Serikali ya Bara

(d)Kiongozi wa Serikali ya Visiwani

Viongozi wa serikali za washirika wa Muungano si lazima waitwe marais, vyeo vyao vitategemea katiba zao. Wanaweza kuitwa Waziri mkuu au waziri kiongozi. Na napendekeza wasiitwe rais ili kupunguza athari za matamshi nchi kuonekana ina marais wengi kama Zaire ya wakati wa Mobutu.wlikuwepo rais wa Katanga, rais wa Bukavu, rais wa Kisangani.

Na huu muundo tayari tunao ni kuuboresha tu hadi sasa Waziri mkuu wa Jamhuri anafanyakazi za bara tu na rais wa visiwani anafanyakazi za visiwani tu.

Ibara ya 67(5) (a) na (b) hazieleweki zinahitaji ufafanuzi.

Ibara ya 69(d) kalenda ya mahakama inamhusu nini rais?

Ibara 69(e) Rais inaidhinisha uwasilishaji wa makisio ya mapato na matumizi ya serikali, bunge na mahakama HAIELEWEKI.

Matumizi ya mahakama yasiidhinishwe na rais, lazima katiba itamke asilimia ya mapato ya nchi yanayoratibiwa na benki kuu yapelekwe kwa shughuli za mahakama ili mahakama iwe huru.anayepaswa kuidhinisha uwasilishaji wa makisio ya matumizi ya mahakama ni jaji mkuu.

Anayepaswa kuidhinisha uwasilishaji wa makisio ya matumizi ya bunge ni spika au katibu wa bunge.hata hivi lazima katiba itamke kikomo cha matumizi ya bunge.

Rais anaweza tu kuwasilisha makisio ya mapato na matumizi ya serikali yake.

Hakuna mapato yanayotokana na bunge wala mahakama hivi ni vyombo ya wanachi kuwalinda mna kutetea haki zao kwa hiyo vinagharimiwa na wananchi wenyewe moja kwa moja na si kwa hisani ya serikali iliyoko madarakani.

Ibara ya 69(3) rais na uteuzi

Vyeo vilivyotajwa katika ibara hii vinatoka wapi kwani ni lazima viwepo kinachotakwa hapa ni kuelezea majukumu ya watu watakaoteuliwa na rais mfano

Rais atateuwa

(a)    Mkuu wa vyombo ya usalama

(b)   Mkuu wa taasisi/wizara  ya …………..(ambayo imetajwa kama sehemu ya mambo ya muungano)

Ibara ya 74 uchaguzi wa rais

(1)    Rais atachaguliwa na wananchi( kwa utaratibu gani?: hii inahitaji ufafanuzi)

 

Asitokane na vyama vya siasa bali agombee kwa aiba yake binafsi (mfano Rais wa Shirikisho la Ujerumani)

 

(2)    Muda wa madaraka ya rais lazima utajwe.

Ibara ya 75 sifa za rais

(f) hakuna ulazima wa kuwa na shahada

(g)si lazima awe mwanachama wa chama cha siasa, anaweza kupendekezwa na chama cha siasa bila kuwa mwanachama wa chama hicho.

Ibara ya 76

(1)    Katiba imetamka miaka mitano ya kipindi cha pili bila kutaja muda wa kipindi cha kwanza.

Ibara ya 77

(1)    Kila chama kitawasilisha jina la mgombea wake hata kama si mwanachama (si kazi ya katiba hii kujua wanachama wa kila chama cha siasa), ikiwa mtu mmoja atapendekezwa na zaidi ya chama kimoja basi huyo atapeperusha bendera za vyama hivyo vilivyompendekeza na kwenye karatasi ya kura kutaonekana muungano huo.

(3      na 4 ) hazieleweki.

Ibara ya 78

(1)    Haki ya kupinga matokeo mahakamani ni ya wote yaani wagombea na wananchi ambao hawakugombea au kupiga kura.Kama haki itabaki kwa wagombea tu kuna huwezekano wa mpinga matokeo kudhuriwa, kuhujumiwa,  kutishwa au kuongwa ili asiendelee na madai yake.

(2)    Siku saba hazitoshi labda kumi na nne.

(4)endapo mahakama husika haitatengua matokeo ya uchaguzi ,Rais hasiapishwe hadi hapo sababu za maamuzi zitakapotolewa.

Ibara ya 79

(3)(a)Rais atashika madaraka hadi siku zitakapoanza kampeni za  uchaguzi mkuu mpya, na katika kipindi chote hicho ataitwa mgombea Urais na si rais.

Ibara ya 80

       (2)atatangaza vita iwapo kundi lililoanzisha vita ndani ya jamhuri halijatokana  linatokana na watanzania wenyewe. Endapo wananchi wenyewe wanaanzisha vita jeshi la wananchi halitatumiwa na rais  kuuwa watu wake.

Ibara ya 84

(6)hoja iungwe mkono na asilimia hamsini na tano

Ibara ya 88

(2)mgombea mwenza atapendekezwa hata kama kwa wakati huo atakuwa ndiye kiongozi mkuu wa mojawapo wa washirika wa muungano.

(4)akishakuwa makamo wa rais ataachia nafasi yoyote aliyonayo katika serikali ya washirika.

Ibara ya 90

(3)(f) Zitakapoanza kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu mpya.

Ibara ya 91

(3)…………………siku zisizozidi kumi na nne baada ya kiti cha makamo wa rais kuwa wazi, rais atateuwa…..

(4) neno ….tena……….limetumika kimakosa.

Ibara ya 93

(1)uteuzi wa mawaziri si lazima waidhinishwe na bunge, kuruhusu bunge kujadili uteuzi kutaibua maswala ya uwiano wa jinsia, kada na kanda wanazotoka.

(2)idadi ya naibu mawaziri haikutajwa.Hata mawaziri kumi na tano wanapatikanaje wakati wizara za muungano ni mambo ya nje, ulinzi,mambo ya ndani na fedha?

Ibara ya 94

(1)(b) si lazima wawe na shahada

Ibara ya 94

(2)(a) madiwani waruhusiwe kuwa mawaziri.

Ibara ya 95

(4)©siku ya kuanza kwa  kampeni za uchaguzi mkuu mpya.

Ibara ya 96

(2)…..ibara ndogo ya (b)…….waziri atatoa ufafanuzi wa jambo husika mbele ya Bunge. Hawezi kuhutubia Bunge.

(3)mawaziri watawajibika kwa pamoja bungeni wakiwakilishwa na nani wakati hawaingii bungeni?

Ibara ya 97

(5)Katika kutekeleza majukumu yake atakuwa na maofisa wa kumsaidia ambao wafanyakazi chini yake…………………………..

Ibara ya 98

(1)Akithibishwa na bunge maana yake Bunge limeingilia muhimili wa serikali. Bunge lipewe tu uwezo wa kumwondoa.

Ibara ya 102

(2)(b) Kiongozi wa Tanganyika

©kiongozi wa Zanzibar

Ibara ya 105

(3)Mkoa kwa Tanganyika na wilaya kwa Zanzibar vimezingatia nini? Je mikoa hii ikiongezeka kwa madaraka ya Rais itakuwaje?.

Ibara ya 110

(2)muswada unaweza kupendekezwa, kuandaliwa na kuwasilishwa  na mtu au kikundi cha watu baada ya kupata kibali cha bunge.

Ibara ya 113

Bunge lisipewe uwezo wa kujiongezea posho wala mshahara.

Ibara ya 115
(2)

Ibara ya 118

(2)(b) Utumishi utakoma punde atakaposhinda nafasi hiyo ya uongozi.

Ibara ya 128

(4)Spika atangaze mali zake kwa umma na awasilishe tamko la mali zake kwa tume ya maadili ya uongozi kabla na baada ya kushika madaraka yake.

Ibara ya 129  ukomo wa madaraka ya spika (si bunge)

(d)hii iondolewe/isiwepo

Ibara ya 132

(d)Uongozi wa ngazi za juu kwa chama cha siasa  kuanzia wapi  wilaya, mkoa au taifa?

Ibara ya 133

(1)Katibu anaweza kuomba kazi akitokea popote alimradi anazo sifa si lazima awe mtumishi wa juu wa katika serikali. Kuna watu hawajapata kuajiriwa na serikali je wasipewe nafasi hiyo.

Ibara 146

(2)Haieleweki maswala gani yanaweza kuwa ya muungano ambayo ni ya madai na jinai?

Ibara ya 151

(1)Jaji mkuu  aajiriwe kama Kenya na kazi zote za uteuzi wa majaji zifanywe  na jaji mkuu

Ibara ya 160

(a)    Haieleweki

Ibara ya 166

©Jaji ,kuu anaweza kumteua jaji yeyote wa mahakama ya rufani kutekeleza kazi za……………….

Ibara ya 184

(8) kwa madhumuni ya ibara ndogo ya (8) nadhani ni ibara ndogo ya (7)

Ibara ya 186 Vyama vya siasa

Vyama vya siasa havitakuwa vya muungano. Kila upande wa muungano utakuwa na vyama vyake na mfumo wake wa uchaguzi.Kama inavyofanyika kuweka serikali ya mapinduzi kwa upande kuwa na chaguzi zake huru ndivyo itakavyokuwa kwa Tanganyika na vyama vitasajiriwa upande mmoja tu wa muungano. Kama majina yatafanana tutaongeza herufi T na Z ili kutofautisha pande za chama kinapotoka.

4 (a)Kila raia anahaki ya kuanzisha chama chake siasa na kunadi falsafa zake ambazo kama zikikubalika atapata wafuasi na kuchaguliwa na kuwa kiongozi katika jamii inayomzunguka. Anaweza pia  kunadi sera zake kama mgombea asiye na chama.

(b)   Muundo wa vyama utaanzia katika ngazi ya tarafa hadi taifa.Katika muundo wa sasa vyama vimekuwa na mashina ya nyumba kumukumi yasiyo na tija kwa taifa badala yake yamekuwa vyanzo vya chuki katika jamii na kuwa vijiwe vya porojo na majungu na unazi wa kisiasa badala ya watu kuongelea sera nzuri za wanasiasa.Muundo wa aina hii umesababisha CCM na CUF kule Zanzibar kuishi kwa uhasama usiokwisha watu wakiamka asubuhi wanakwenda kunywa ulojo wengine maskani ya CCM na wengine ya CUF matokeo ni kuzungumza ya jana badala ya kupanga mambo ya kesho. Katika muundo wa tarafa tutaondoa siasa za chuki na tutajadili sera za vyama bila ubaguzi kama tunavyojadili mpira wa Simba na Yanga bila chuki. Uzoefu unaonyesha kwamba muundo wa vyama kuanzia kwenye mashina umesababisha baadhi ya familia kujiita kwamba ni za chama fulani bila kujari manufaa ya vyama hivyo kwa taifa.

(c)     Katika mundo wa vyama vya siasa itakuwa ni marufuku kwa watoto chini ya miaka kumi na nane kujihusisha na siasa. Katika siasa za sasa kuna watu wanaitwa chipkizi wanabatizwa bila ridhaa yao kuwa wanachama watarajiwa wa vyama fulani , huu ni muundo uliopitwa na wakati wa kulazimisha mambo kwa ulaghai na hauna tija kwa taifa.Muundo wa nyumba kumikumi ulikwekwa ili kuwezesha watawala wa zama zile kudhibiti wageni kuingia kiholela ndani ya nchi yetu. Kwa sasa tunazo teknolojia za kutambua wageni wanaoingia nchini bila kuhitaji wajumbe wa nyumba kumi.

(d)   Hakuna chama kitaruhusiwa kuwa na bendera zenye rangi zinazofanana na rangi za bendera ya taifa au za vilabu vya Simba na Yanga.Katika siasa za sasa kuna watu wengi wanaopumbazwa na rangi hizi badala ya watu kuchagua sera wanachagua chama chenya rangi za Simba au Yanga wanadanganywa na wazushi kwamba chama chenye bendera ile ni cha timu fulani.Kwa kuwa timu ya Yanga ni kongwe kuliko CCM, chama hiki itabidi kitafute rangi zingine endapo Katiba mpya itaruhusu vyama vilivyopo kuendelea kuwepo ingawa mimi napendelea tuanze siasa zetu kwa kuunda upya nyama vyetu hata kama majina yanaweza kuwa yaleyale lakini rangi za bendera na muundo lazima vibadilike.

(e)    Endapo chama kitashinda chaguzi mfululizo na kukaa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi na nane kitasimamishwa kushirirki uchaguzi utakaofuata kwa muda wa miaka mitano ili kupisha kizazi kingine kushika madaraka.Wanasiasa wa chama kilichosimamishwa hawataruhusiwa kuhamia vyama vingine.Aidia hapa ni kuzuia chama Fulani kutawala vizazi zaidi ya kimoja  mfululizo.

(f)     Muundo wa vyama usiangalie tofauti za umri wala jinsia kama ilivyosasa. Sioni kama kuna haja ya kuwa na jumuia za vijana au kina mama huu ni ubaguzi.Kiongozi katika chama apatikane kwa aiba yake. Mfano ni kule Ujerumai ambapo ilimchukua Chansela Angela Mekel muda mrefu kugombea na kupata kiti katika chama chake cha CDU lakini wakati ulipofika watu walimchagua.Ubaguzi wa aina ya umri uliigawa CCM mwaka 1995 kati ya Kikwete ambaye alikuwa chaguo la vijana na wagombea wengine waliokuwa na umri mkubwa.Tunataka tuondoe hali hiyo.Pia viongozi wastaafu wanapaswa kutoshawishi viongozi wapya ili kupisha fikra mpya za viongozi wapya wanaochaguliwa.

Ibara ya 188

Ibara ya 194

4(b) awe na uelewa mkubwa kuhusu haki za binadamu na rekodi  ya kutetea na kulinda haki za binadamu, kuwa na shahada ya sheria tu hakumfanyi mtu apende haki za binadamu.

Ibara ya 196

Muda wa wajumbe wa tume wa miaka mitatu ya vipindi viwili umezingatia nini? Iwapo mtu bado anafaa kwa kazi hiyo ina maana asipewe tena nafasi hiyo?.

Ibara ya 202

1(d) mdhibiti na mkaguzi atawasilisha bungeni ripoti kupitia kwa nani?

4 na 5 kama taarifa itapita kwa Rais kabla ya kwenda bungeni inaweza kufanyiwa marekebisho ili kumpendeza rais.

Ibara ya 203

(1)    Kwanini ni miaka saba tu na haiongezwi?

 

Ibara 213

1.       Serikali kabla ya kukopa lazima itoe taatrifa bungeni kuhusu nia ya mkopo huo kwa kutekeleza ibara ya (2) kwa mikopo ya nje.

Ibara 214

(1)    Serikali za washirika ziwe na uwezo wa kukopa mikopo katika benki za ndani tu.

Ibara 215

(a)    Ushuru wa bidhaa kisiwe chanzo cha mapato ya Muungano. Serikali ya Muungano isijihusishe na biashara.

Ibara ya 217 BENKI KUU

Huu utakuwa mhimili huru kabisa ambao utashirikisha asasi na taasisi zote za fedha.Gavana wa fedha atachaguliwa na wachumi wenzake baada ya kuomba na kusailiwa na Tume ya ajira za juu ya taifa katika utaratibu ambao wachumi wataona unafaa na hatakuwa mteule wa rais.

BOT lazima iendeshwe na kuwa benki kubwa kama IMF,ADB, au WB kwa kutumia rasilimali zetu hata iweze kutoa mikopo kwa nchi nyingine punde uwezo ukiruhusu kwa manufaa ya taifa.Hii inawezekana kwa sababu mfumo wa BOT ni sawa na wa benki zingine isipokuwa tofauti ni kwamba wateja wa BOT ni mabenki badala ya watu binafsi.Kama CRDB inakopesha wateja wake kwanini BOT isikopeshe nchi kama Komoro na ikatoza riba.

Aidia hapa nikuipa uhuru BOT ili kuiwezwesha kumiliki uchumi moja kwa moja bila kuingiliwa na na wanasiasa. Uganda walipata kuwa na rais Idd Amin ambaye alimwamuru  gavana wa benki ya Uganda ''print more money''. Hapa Tanzania rais Nyerere ambaye hakuwa mchumi alikataa kugeuka jiwe aliposhauriwa na gavana Edwin Mtei kuhusu kukubali kushusha thamani ya shilingi dhidi ya dola ya kimarekani ili kukabiliana na uchumi uliokuwa umeathiriwa na vita ya Kagera. Laiti gavana Mtei angekuwa na nguvu za kikatiba yote haya yasingetokea na kama ungefanya makosa kwa kushusha thamani ya shilingi bila weledi angeadhibiwa kikatiba.Katiba hii mpya impe gavana madaraka ya mwisho kuamua mambo kama hayo na mahakama peke yake yaweza kutumika kuhoji uweledi wa maamuzi yake.

BOT itatoa kwa uwazi mwenendo wa uchumi wetu kila baada mwisho wa mwezi. Itakusanya kodi zote kubwa zenye VAT, itasimamia kodi zinazitokana uwekezaji toka nje kama utalii,biadhara za kimataifa, mahoteli makubwa, bandari,biashara za ndege, meli, madini yote, uwindaji. Katika katiba ya 1977 baadhi ya wanasiasa  wamekuwa wakishirikiana na wawekezaji na kuwakingia kifua ili kuwawezesha kupora uchumi wa taifa.Kampuni moja simu za mkononi inabadili jina kila inapoona kipindi chake cha msamaa wa kodi  kinakaribia kumalizika, BOT itakomesha mianya ya namna hii.

Mimi nikiwa mzalendo wa kisasa ninaamini kabisa kuwa nchi yetu inao wataalamu wa uchumi wazuri ambao tukiwapa uhuru wa kutenda kwa weledi watapeleka uchumi wetu kwa kasi ya ajabu kimaendeleo.Wanazo au kama hawana waweke sheria zao za weledi na mchumi akiteteleka anadhibiwa kisheria.

Biashara zote za kununua rasilimaliagizwa (import goods) ambazo Mungu akuijaria nchi yetu zisimamiwe na BOT moja kwa moja. Bidhaa kama petrol badala ya kuachwa kwa kuagizwa kibiashara na watu binafsi na kuilangua kwa wananchi ziwekwe katika kundi la bidhaa muhimu kwa taifa na zisimamiwe na BOT kutegemea na hali ya uchumi wa nchi.Nchi kubwa kama Marekani zimejiwekea utaratibu wa kuzipiga vita nchi za kiarabu na kuzipora mafuta na wala si mabepari na mabwanyenye wa huko walioachiwa kuagiza mafuta.Hii inasaidia kumonita bei ya mafuta ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi kwa nchi zinazotumia nishati hiyo.Vivyohivyo rasilimali zote ambazo hazipatikani Tanzania hazitakuwa sehemu ya kujitajirisha kwa watu wachache badala yake ziratibiwe na BOT  moja kwa moja kutegemea na ukuaji wa uchumi wetu.

Ushuru wa forodha (bidhaa toka nje ya nchi) ni kazi ya BOT. Mikataba yote ya kimataifa kuhusu fedha, mikopo, misaada ya fedha toka nje ya nchi na mifoko ya fedha ya kimataifa zisimamiwe moja kwa moja na BOT kutegemea na uchumi wa nchi.Hakuna mwanasiasa atakayeruhusiwa kwenda nje ya nchi kuomba misaada kama tunavyoona marais wetu walivyofanya. Rais wa nchi unakwenda kuomba msaada kwa niaba ya watu wako bila ridhaa yao ni kuidhalilisha nchi.

Mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi iandikwe kwa lugha ya Kiswahili na wageni walazimike kujua lugha hiyo.Mikataba yote ya aina hiyo itangazwa kwenye vyombo vya habari ili kila mwananchi ahoji uhalali wa masharti ya mikataba.

 

 

 

Ibara ya 223

Jeshi la wananchi wa Tanzania

Itakapokuwa pametokea ombwe la uongozi katika nchi kwa kiasi ambacho raia wanashindwa kuendesha majukumu ya kila siku itakuwa ni wajibu wa jeshi kushika mamlaka na kurejesha utulivu ili katiba hii ifuatwe.jeshi litakuwa katika hatamu kwa kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Ibara ya 232

(1)    Kusiwe na polisi wa washirika wa Muungano.

Ibara ya 235

Kusiwepo na idara za usalama za washirika wa Muungano.

Ibara 238 Jumuia ya madola haieleweki

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments