[wanabidii] Dr. LWAITAMA KUDHALILISHWA KATIKA PRECISION AIR

Monday, January 27, 2014
Kwa ufupi alitumia kiti cha emergence exit wahudumu wakampa maelekezo ahame kwa kutumia lugha ya kiingereza akajifanya haelewi akagoma kuhama kiti akawambia wampe maelekezo kwa kiswahili. 

Wahudumu waliita polisi wakamshusha toka kwenye ndege wakimtuhumu kusababisha vurugu.

Safari yake ilikwama, na kudhalilishwa.

Hapa nawakosoa watoa hoja kusapoti kitendo cha kukubali ukoloni mamboleo.

Nyote mnaotetea ukoloni mamboleo mnasaliti nchi yetu.

Dr. Lwaitama ni mwelewa kuliko ninyi mnaombeza. Ni jasiri na mzalendo.

wengine ni form four failure mnajifanya kumwona Dr. Lwaitama mjinga au mtu wa kuvuruga wengine!!

Mnajua Socrates alivyofikisha ujumbe wake wa Falsafa katika Ancient Greece??

Aliwamulika watu mitaani kwa torch mchana jua likiwaka akiwahubiri fikra zake hadi aliponyongwa na serikali kwa kufundisha watu ukweli.

Aliwaeleza watu watafakali maisha yao yaliyojaa giza wakijifanya wanajua ilihali hawajui na wakiwa wamejaa uovu.

hadi leo Socrates anakumbukwa na dunia nzima inajifunza mengi sana kutoka kwake Socrates ila serikali ya nchi yake walimnyonga kwa kille walichosema anapotosha wananchi as same as Jesus Christ alivyokuwa acused ili hali alitetea kweli ya Mungu(Kwa wakristu).

Mnaodhani Dr. hakujuwa kiti alichokitumia haikuwa sawa? ninyi mnapepesuka tu mkiwa masikini katika fikra zenu.

Kswahili ni lazima tukitetee kwa njia zote na ktk ndege ni bora zaidi kutokana na wageni wengi kutumia usafiri huo. ninyi mnaleta umbumbumbu wenu mkijifanya kiwa kiingereza ni bora kuliko kiswahili.

Dr. amefungua ukurasa mpya wa kutetea utamaduni wetu Watz.

Kiswahili ni tunu na nembo ya nchi yetu lazima tulinde lugha yetu kwa gharama na kujitoa.

Ni mhm sana tutafakali kwa uzalendo hatua aliyoichukua Dr. Lwaitama!!! Sio hisia ni hali halisi...!!

Tufikilie kwa mapana, tupenda na tuwe wazalendo wa nchi yetu.

Wewe unamtazamo gani?

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments